skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na: Mwandishi Wetu – DODOMA

Kamati ya Bunge ya Ustawi wa Maendeleo ya Jamii imempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ustawi wa vijana na Watu wenye Ulemavu kujikwamua  kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 15, 2023 bungeni na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq kwenye kikao cha kamati cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana pamoja na utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Aidha, Mhe. Fatuma Toufiq amesema kamati hiyo itaendelea kuishauri Serikali kuendelea kuongeza wigo wa kuwezesha vijana wengi zaidi kupata mikopo, fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Mendeleo ya Jamii Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)  leo tarehe 16 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa kamati hiyo Bi. Aziza Kheir.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako ameeleza kuwa Ofisi yake imefanya maboresho ya mwongozo wa mfuko huo mwaka 2023 ili kupanua wigo wa viwango vya mkopo inayotolewa sambamba na kumwezesha mtu moja moja kukopa badala ya kikundi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa mwaka 2022/23 kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 16 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu.

Naye, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu amesema kuwa, ofisi hiyo imetenga Sh.Bilioni moja katika mfuko wa Watu wenye Ulemavu kwa ajili ya utekelezaji wa afua mbalimbali za kundi hilo.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma