skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Matinde Nestory, Mwanza

Viongozi wa kamati ya Amani Mkoani Mwanza wamekutana katika kikao Cha pamoja Cha kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupanua wigo na kujenga mahusiano ya kidipromasia na kuendeleza miradi ya kimkakatii iliyoachwa na hayati Dr. John Pombe Magufuli. 

Akizungumza na viongozi wa madhehebu ya dini ya kiislam na kikristu katika ukumbi wa Victoria uliopo Mkoani Mwanza Askofu Charles Sekelwa ambeye ni kiongozi wa kati hiyo amesema kuwa viongozi wa kamati ya amani wamekutana kwa ajili ya kumpongeza, kumshukuru pamoja na kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita.

Askofu Sekelwa amesema kuwa Rais Samia amepanua wigo katika kulijenga Taifa la Tanzania na kuleta mahusiano ya kidipromasia baina ya nchi na nchi na kulifanya Taifa la Tanzania kutambulika duniani kote kupitia filamu ya Royal tour.

“Sisi Kama kamati ya Amani mkoa wa Mwanza tumejiridhisha, tumechunguza, tumejipatia taarifa sahihi na tunayoyasema ndivyo yalivyo”amesema Askofu Sekelwa.

Akitoa pongezi kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinatotekelezwa nchini, Askofu Sekelwa amesema kuwa serikali ya Tanzania imetoa shilingi bilioni 264 kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi wa ndani na nje ya nchi, amelipa madeni zaidi ya trion 11, na kupitia filamu ya Royal tour watalii wameongezeka Tanzania.

Viongozi wa kamati ya amani mkoa wa Mwanza Shekhe Hassan Kabeke (wa pili kushoto), Askofu Charles Sekelwa (wa pili kulia)wakiwa katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari jijini Mwanza

Aidha Kamati ya amani imepongeza serikali kwa kuikumbuka Idara ya maji kwa kutoa shilingi bilioni 88 kwa ajili ya wakazi wa Mkoa wa Mwanza, kupandisha mshahara kufikia 23.3%, kusimamia haki za binadamu na utawala bora.

Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke amesema kuwa wanampongeza Rais Samia kwa kupokea tuzo ya mjenzi bora iliyotolewa nchini Ghana, kutoa bilioni 100 kwa ajili ya kupunguza makali ya mafuta pamoja na kutoa milioni 10 kwa kila Mkoa kwa ajili ya kuwasaidia wamachinga.

Nae mshauri kamati ya amani Mkoa mchungaji  Dkt Jacob Mutashi amesema kuwa viongozi wa dini ni  wabia na serikali katika kukutana na kujadili amani ya Tanzania.

“Viongozi wa dini tuna watu katika nyumba za ibada tunaheshimika kwa sababu tunachokiagiza waumini wanafanya, niombee kila agizo lolote ambalo Rais  Samia akitaka  liwafikie watu kwa haraka na liwe na matokeo ya haraka, viongozi wa dini wahusishwe hata katika kupewa Elimu” amesema Dkt Mutashi.

Kwa pamoja viongozi wa kamati ya amani inayoundwa na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali ya dini ya Wakristo na Walamu wameutumia mkutano wao kuwaomba watanzania kujitokeza katika katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma