WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua jengo la wagonjwa wa dharura kwenye hospitali ya wilaya ya…
Na Idd Mashaka.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Morogoro wamepewa mafunzo maalumu ya uraia na Maafisa uhamiaji kutoka Morogoro Katika semina iliyofanyika Katika chumba cha tathimini chuoni hapo asubuhi ya leo.
Mafunzo hayo ambayo yamehusisha aina mbalimbali za uraia nchini Tanzania yamelenga kuwaongezea ufahamu waandishi wa Habari kuhusu masuala mazima ya uraia na sheria za uraia.
Akizungumza kuhusu aina za uraia Mwana Sheria wa idara ya uhamiaji Samuel Mwakatage amesema “ zipo aina tofauti za uraia nakuziainisha kwakusema kuna uraia wa kuzaliwa,kuhamia au kuandikishwa na uraia wa kurithi” huku akiongeza aina za kukoma kwa uraia.
Akifafanua kuhusu uraia wa kuhamia amesema muombaji wa uraia anapaswa kuomba nafasi ya uraia nchini Tanzania ikiwa ameishi Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi (10) isipokua kwa mwanamke alieolewa Tanzania ambae sheria inamruhusu kuomba uraia hata kabla ya kutimiza miaka kumi.
Pia ameongeza kwakusema Tanzania haina uraia pacha (yaani dual citizenship) nahiyo nikwamjibu wa sheria ya uraia sura ya 357 kifungu namba saba (7) rejeo la mwaka 2002.
Akijibu swali la mshiriki wa semina lililohoji “mtanzania ambae awali alihamia nchi nyingine na baadae akataka kurejea Tanzania inakuwaje”?amesema anapaswa kufuata taratibu zote zakuomba uraia kwa mjibu wa sheria.
Kwa upande wao wanafunzi wameguswa na semina hiyo ikiwa nipamoja na kujifunza namna ya kumjua jirani yako Kama wanavyoeleza hapa Isabella Julius na Lucas Josephat.
Hata hivyo Maafisa hao wehitimisha kwakusema jukumu lao kubwa nikusimamia na kudhibiti watu wanaoingia na kutoka nchini sambamba nakutoa elimu ya mjue jirani yako kwa wananchi wa Tanzania.