Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Robert Gabriel amewaomba wananchi kutokomeza ukatili wa kijinsia ambao unaanzia katika ngazi ya familia kwenda kwenye jamii.

Ameyasema haya katika maadhimisho ya ukatili wa kijinsia ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mwanza yenye kauli mbiu “Ewe mwananchi komesha ukatili wa kijinsia sasa”
Madhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Nyamagana jijini humo, yamehudhuriwa na shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana la KIVULINI, Plan International,Wote sawa, Railway Children na Source Children Village wote wakiwa na lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia.
RC Gabriel ametaja mikoa ya Kanda ya ziwa inayoongoza kwa ukatili wa kijinsia ikiongoza mikoa ya Shinyanga na Mara 78%, Kagera 67, Geita 63%, Simiyu 62% na Mwanza asilimia 60%
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani humo SACP Ramadhani Ng’anzi amesema kuwa siku kumi na sita za kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia jeshi la polisi linapinga ukatili wa aina yoyote ambao unafanyika dhidi ya wanawake na watoto ambao umeathiri utendaji kazi wao na kutokujiamini katika kutetea haki zao.
Naye Afisa Mwandamizi wa shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana KIVULINI Grace Mussa amesema vitendo vya unyanyasaji wa watoto unatakiwa ushughugulikiwe kwa usiri kwa masaa ishirini na nne na kwa weledi ili kulinda utu wa watoto.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ofisi ya taifa ya takwimu NBS mwaka 2015 na 2016 inaonesha kuwa mikoa ya kanda ya ziwa inaongoza nchini kwa kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia.
Mwandishi: Matinde Nestory
Mhariri: Adela Madyane