skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Vyombo vya habari nchini Tanzania vinaongozwa na sheria mbalimbali ambazo husimamiwa na wizara kuu mbili yaani Wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo pamoja na Wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari.

Wizara inayodhibiti ubora na maudhui kwa vyombo vya habari vya kielectroniki (Radio, Runinga na mitandao) ni wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari ambapo mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA ndiyo kiranja mkuu wa kuhakikisha ubora wa utangazaji na pia usimamizi wa maadili.

Katika Bajeti ya mwaka 2021/2022 Wizara hiyo imetaja vipaumabele vingi vya kisekta na kutenga fedha katika bajeti kwa ajili ya kuhudumia shughuli za wizara hiyo. Je! Kuna matumaini ya nafuu ya uendeshaji wa vyombo vya habari, mawasiliano ya simu na mitandao ya kijamii? Link iliyopo hapo chini ina hotuba nzima wa makadirio ya mapatoo na matumizi ya wizara hiyo tafadhali bofya hapa uisome

Buha FM radio tunampongeza waziri Dr. Faustine Ndungulile kwa kuwasilisha makadilio ya mapato na matumizi na pia kwa Bunge kupitisha bajeti hiyo. Ni matumaini ya watanzania na watumiaji wa vyombo vya mawasiliano ikiwemo Radio kuwa mwaka 2021/2022 utakuwa ni mwaga wa mageuzi chanya katika tasnia ya habariii na mawasiliano.

Kazi Iendelee”

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma