Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika inaadhimisha miaka 30 tangu kuasisiwa huku kukiwa…
Na. Mwandishi wetu, KIA
Serikali ya Tanzania imefanikiwa kutatua changamoto ya hitilafuu ya taa za kuongozea ndege katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro ambayo ilisababisha wageni walikuwa wakisafiri kwa shirika la ndege la Uholanzi KLM kushushwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda
Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa serikali Bw. Gerson Msigwa, tukio hilo lilitokea jana majira ya jioni baada ya taa hizo kushindwa kufanya kazi katika kiwango kinachotakiwa na kupelekea usumbufu kwa ndege zilizotakiwa kutua katika uwanja huo
Kuhusu Uvumi wa kufungwa kwa uwanja huo Bw. Msigwa amebainisha kuwa tayari marekebeishoo yamefanyika na ndege zinaendelea kuutumia uwanja huoo kama kawaida na kwamba abiria walioshushwa nchini jirani ya Uganda taratibu za kuwasafirisha kwenda Kilimanjaro zinaendelea
Video hapa chini inafafanua kuhusu taarifa hizo