skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Zipo hadithi nyingi sana kuhusu Mkoa wa Kigoma na kabila la Waha, vitabu mbalimbali vimeandikwa kuuzungumzia mkoa wa Kigoma uliofahamika zamani kwa jina la BUHA. Watunzi mbalimbali akiwemo Mwalimu Chubwa, Kipfumu na wengine waliandika kuhusu Mila na desturi za kabila la Waha. Aidha Msanii kutoka Kasulu Mzee Francis Nyakamwe naye ameandika mengi kuhusu misemo, lugha na nyimbo za Kiha.

Kigoma mwisho wa reli

Pamoja na maandiko hayo, Mhandisi Amoni Ntimba naye amedadavua kuhusu BUHA na mahusiano ya kikanda, lugha na majina ya maeneo.

Ntimba anaandika kuwa = TOFAUTI YA WAHA NA MAKABILA JIRANI YA WAHANGAZA, WASHUBI, WARUNDI NA WANYARWANDA. Waha ni kabila la Kibantu linalopatikana Mkoani Kigoma, Tanzania, ktk wilaya zote za Mkoa wa Kigoma, kumekuwa na kasumba ya kuwaita WAHA kuwa ni Warundi/wacongo sana ktk nchi yetu ya Tanzania Kitu ambacho si sahihi Kihistoria na hata Kwa kufata Tawala za Zamani kabla ya UKOLONI. 
Kama ilivyo Kwa  WAHAYA,WANYAMBO,WAKIGA,WANYORO na WANYANKORE kuwa na Chimbuko moja na Lugha zinazoshahabiana, Au WASUKUMA na WANYAMWEZI, vile vile Waha pia ni Kundi la Wabantu lenye Asili moja na Jirani zao wa Burundi, Wahangaza,Wanyarwanda na Wafumbira na hii tunaipata kutokana na LUGHA za Makabila hayo kufanana kwa Takribani Asilimia 85-90%, Majina kufanana na hata KOO(CLANS) nyingi kufanana na hata majina ya Vijiji, Mfano 1;kijiji cha Kalinzi (Kigoma),Mkalinzi(Ngara)
2;mnanila(kigoma) na Munanira(Kayanza-Burundi)
3: Mji wa Kigoma kusini mwa Rwanda
4; Kiremba kijiji (Manyovu, Kibondo) na Kiremba mji huko Bururi (Burundi) 
5; Muganza(Ngara), Muganza(Kasulu) , Muganza (Butare-Rwanda), 
6; Nkundusi(Rulenge-Ngara) , Nkundusi(Kasulu),  Nkundusi (Mwaro-Burundi).
7; Kanazi ( Kasulu),  Kanazi(Ngara), Kanazi( Bubanza-Burundi). 
Kasulu (Kigoma),  Kasulu (Makamba-Burundi) 
WATAALAMU wa Lugha huamini Lugha za KIHA,KIHANGAZA,KIRUNDI NA KINYARWANDA /KIFUMBIRA Ni Lahaja za Lugha MOJA ila zimetofautiana baadhi ya Maneno na Matamshi kutokana na kuhama hama kwa Wabantu hawa. 
KUTOKANA NA KUHAMA HAMA, kila Kabila lilisimika Makazi sehemu yake na kuanzisha Tawala zao za Jadi, Eneo la BUHA liligawanyika ktk Tawala Zifuatazo 1:HERU,uliotawala eneo kubwa la KASULU na BUHIGWE chini ya Ukoo wa WAKIMBIRI, Malkia THERESIA NTARE alitoka utawala huu uliokuwa na makao makuu Heru juu, Kasulu. 2: NKALINZI, ulijumuisha eneo la Kalinzi kuelekea Kigoma mjini na mwambao wa ziwa Tanganyika, Chini na Ukoo wa Wajiji, Mfalme wa mwisho aliitwa Mwami RUSIMBI, makao makuu yalikuwa Kalinzi, kigoma. 3: MUHAMBWE4: BUYUNGU 5: HERU BUSHINGO nkNkTAWALA hizi za WAHA zilianza miaka mingi kabla ya kuanzishwa kwa Tawala za BUGUFI (NGARA) na Burundi, na hata Wafalme wa Tawala hizi walitoka koo tofauti na Tawala jirani Mfano HERU Kingdom (Himaya) ilitawaliwa na ukoo wa WAKIMBIRI, NKALINZI kingdom (Himaya) Ilitawaliwa na ABAJIJI, MUHAMBWE na BUYUNGU zilitawaliwa na Ukoo wa ABAHUMBI nk, tofauti na BURUNDI Kingdom ilitawaliwa na ukoo wa ABAGANWA, RWANDA ukoo wa ABANYIGINYA, na BUGUFI (NGARA) ilitawaliwa na ABAGANWA inasemekana hata Mfalme wa kwanza wa Burundi alitokea Buha Uwezekano wa hilo ni mkubwa kwa Sababu Maeneo ya MATYAZO na Nyarubanda KIGOMA Kuna Waha wa Ukoo wa WAGANWA wengi Sana na ndio ukoo uliotoa Wafalme Burundi, Tawala za BUHA zilikuwa na Wafalme wake na Majeshi yao, lakini walishirikiana sana na jirani zao wa Burundi na Kagera kwa Kuoana na kusaidiana Vitani, Mfano kipindi cha mfalme wa Burundi (Mwezi Kisabo) akipigana na Wajerumani aliomba msaada kwa Jeshi la BUHA na Bushubi kumsaidia wapiganaji, Pia warundi walitumia ardhi ya BUHA kupigana na Wanyamwezi, pia Mfalme NTARE (Kiitabanyoro) wa Karagwe alisaidiwa na jeshi la Buha kuwashinda Wanyoro walipovamia Karagwe nk. 
KIHISTORIA Mfalme wa Burundi hakuwahi Tawala eneo la BUHA Tofauti na maeneo ya BUYOGOMA aliyoyateka na kuyajumuisha Burundi. WAHA walikuwa na Utawala Thabiti uliojumuisha Mfalme wa Wasaidizi wake (Watwale) waliosimamia utawala ktk Vijiji na Jeshi la kulinda ardhi yake. 
Ukiangalia JIOGRAFIA Ya Kigoma, Waha walipakana na warundi Magharibi, Mashariki sehemu kubwa walipakana na PORI LA MOYOWOSI, Na kwa uchache Kaskazini na kusini walipakana na Wasubi,wahangaza na kusini wafipa, tongwe na Manyema, hivyo kutokana na mpaka mrefu Kati ya Waha na Warundi, muingiliano ulikuwa ni mkubwa hasa Kwa Waha wa Milimani ndio maana Koo nyingi za Waha wa Milimani hufanana na jirani zao wa Burundi Mfano ABALAGANE, ABAJIJI, ABACHABA, ABAZIGABA, ABALIMA, ABATWA, ABASHINGO, ABABANDA,ABAVUMU nk ziko pande zote za mpaka, hii ni kutokana na kuhama hama kabla ya UKOLONI Na mipaka kutengwa, Sawa tu na Wajaluo wa Kenya na Tanzania au Wamasai, lakini Wahusika wa koo Hizo upande wa Tanzania walijiita WAHA na ilhali jirani zao wakijiita WARUNDI, lakini pia Kuna koo za Waha wa Milimani ambazo haziko kabisa BURUNDI Mfano Abanyongozi, Abakimbiri, Abanyakasambiro nk Pia Kuna baadhi ya KOO za WAHA zenye CHIMBUKO moja na WANYAMBO/ANKOLE/WAHAYA Mfano koo za WAKIMBIRI, WAZIGABA, WAYANGO/WAZILANKENDE, WACHABA,WASINDI nk. Hizi koo zilitokana na Muingiliano wa Waha na Makabila ya Kagera na Ankole Uganda. 
WAHA ni Kabila kubwa na Wazawa wa Mkoa wa Kigoma, kufanana kwao Lugha kwa kiasi kikubwa (85-90%) na jirani zao ni Sababu ya Ubantu wao Ila haiwafanyi wawe Warundi/wanyarwanda Wala Wahangaza. Kumuita MUHA kuwa ni Mrundi au Mnyarwanda ni sawa na Kumuita MUHAYA kuwa ni Mnyambo, Mnyankole au Mkiga, Kitu ambacho si sahihi, Kila kabila lilikuwa na HISTORIA yake na Wafalme wake. Na WAHA ndilo kabila pekee Tanzania lililokuwa na Chief Mwanamke, Mwamikazi Theresia Ntare toka HERU na lina historia ya kuwashinda Wangoni ktk mapambano walipovamia ardhi ya BUHA.
MUHA ni mzawa halisi wa BUHA(KIGOMA) na Mrundi, Mhangaza, Mnyarwanda na Mfumbira ni ndugu na jirani za MUHA Sababu walitokana na Kundi Moja la Wabantu lililozaa MAKABILA tajwa hapo juu. IM PROUD TO BE FROM BUHA LAND.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma