skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Mawaziri wa mazingira kutoka nchi za ukanda wa ziwa Tanganyika leo wamekutana mjini Kigoma kwa ajili ya kujadili mikakati ya kunusuru ziwa Tanganayika dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mkutano huo wa kikanda umezinduliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Philpo Mpango ambapo pamoja na mamb mengine amewaagiza vmawaziri hao kuweka mikakati mahususi ya matumizi endelevu ya ziwa hilo linalohidumia watu Zaidi ya milioni 10

Dr. Mpango amezitaka nchi zinazozunguka ziwa hilo kutengeneza sera ya pamoja ya usimamizi wa mazingira sambamba na kutunga sheria zinatazotumika kuratibu matumizi yam aji, ardhi na misitu ili kuepuka athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Dr. Mpango amebainisha kuwa licha ya ziwa Tanganyika kuwa na uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa cha saamaki kwa sasa linazalisha kiasi kidogo jambo linalotajwa kutokana na sababu za uvuvi haram una athari za kimazingira

Dr. Philipo Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania akihutubia mkutano wa mawaziri na wadau wa mazingira ukanda wa ziwa Tanganyika.

“Ziwa hili lina uwezo wa kuzalisha kiasi cha zaidi ya tani milioni moja na nusu za Samaki lakini kwa sasa linazalisha chini ya kiwango chake kwa takribani tani laki tano tu,” amesema makamu wa Rais Dr. Mpango

Akitoa taarifa ya mwenendo wa ushirikiano wa kikanda katika kuhifadhi mazingira katika bonde la ziwa Tanganyika, naibu Waziri ofisi ya makamu wa Rais anayeshughulikia muungano na mazingira Bw. Hamad Chande amekiri kuwepo na tija pamoja na kuwepo na changamoto kadhaa

Chande ametaja baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na kuandaliwa kwa mipango ya pamoja ya ulinzi na uhifadhia wa bonde kwa ujumla pamoja na uanzishwaji wa sekretarieti ya kikanda inayoratibu shughuli za jumuiya hiyo ya nchi za bonde la ziwa Tanganyika

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya mawaziri hao Bw. Collins Nzovu ambaye ni Waziri wa mazingira na uchumi wa kijani kutoka Zambia ametaja masuala mhimu ya kuzingatiwa ili kulinusuri ziwa Tanganyika.

Mhe. Nzovu amesisitiza kuwa Kila taifa linatakiwa kuchukua hatua za kulilinda ziwa hasa kwa kudhibiti uharibifu wa mazingira, kudhibiti upasuaji wa mbao na uchomaji wa mkaa, kudhibiti uvuvi kuhakikisha kuna kilimo endelevu, hii inapaswa kufanywa na kila nchi

Mawaziri kutoka Burundi, DRC, Tanzania na Zambia pamoja na mambo mengine wamekubaliana kuongeza juhudi za kudhibiti uharibifu wa mazingira ikiwemo kuzuia kilimo katika miinuko na bonde la ziwa, ukataji miti kwa ajili ya mbao na mkaa, pamoja na uvuvi haramu.

Serikali ya Zambia imepongezwa kuwa kuwa nchi ya kwanza kutunga sheria ya kudhibiti upasuaji wa mbao na uchomaji mkaa katika misitu na hifadhi ya bende la ziwa Tanganyika na nchi nyingine zimepewa wito wa kufanya hivyo.

Mwandishi: Prosper Kwigize, Kigoma

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma