skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Adela Madyane-Kigoma

Mkuu wa wilaya ya Uvinza Dinnah Mathamani (katikati) akiambatana na vingozi wa mradi wa Tuungane, amekagua ujenzi wa jengo la kukusanya, kuchakata, kusindika na kufungasha samaki na dagaa wa ziwa Tanganyika  lililopo kata ya Buhingu wilayani Uvinza  lenye thamani ya shilingi milioni 167.

Jengo hilo limejengwa na shirika la The Nature Conservancy (TNC) kwa lengo la kupunguza upotevu wa mazao hayo kwa kuyaongezea thamani ili yaweze kukidhi vigezo vya kuuzwa katika  soko la kimataifa na kuongeza pato kwa wananchi na wilaya kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Mradi Lukindo Hiza amebainisha kuwa ujenzi wa mradi huo umetokana na dhamira ya shirika hilo kuunga mkono juhudi za serikali katika kusaidia jamii kupambana na umasikini kwa kuongeza thamani ya mazao na kupanua wigo wa soko la mazao ya uvuvi

Kwa upande wake afisa uvuvi wilaya ya UvinzaHaroun Chanda amesema  hatua ya awali ya ujezni huo umakamilka huku hatua inayofuata ni ujenzi wa jengo la barafu,ununzi wa nyavu pamoja na jengo la stoo na kwamba mpaka ukamilifu wake utagharimu takribani milioni 360.

Mpaka sasa sekta ya uvuvi inachangia shilingi milioni 200 kwenye pato la halmashauri kwa mwaka na katika wilaya hiyo kuna jumla ya wavuvi 2800.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma