skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki, Bariadi 

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga ametoa maagizo akimemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa kwenye halmashauri hiyo inakamilika kwa wakati na  kwa viwango vinavyotakiwa

Ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua miradi inayotekelezwa kwenye maeneo tofauti tofauti kwenye halmashauri hiyo huku akiongeza kuwa fedha zinazoletwa na zitakazoletwa lazima miradi ikamilike kwa fedha zilizoletwa.

Mbali  na maagizo hayo amesisitiza kuwa kiu ya serikali ni kuona mapato yanatokana na makusanyo ya halmashauri yanatumika kujenga miradi mipya na sio kutumia fedha zinazotokana na mapato hayo kukamilisha miradi ambayo serikali kuu imeshaleta fedha zake kwa ukamilifu.

“Mhakikishe mafundi wanafanya kazi ikiwezekana mchana na usiku lazima twende na muda, suala LA utekelezaji wa miradi kwa muda na kwa viwango vinavyotakiwa hilo nitalisimamia wekeni taa mafundi wafanye kazi usiku na mchana”amesema Simalenga 

Tazama video ya Mkuu wa wilaya ya Bariadi Simon Simalenga akitoa maagizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo mhandisi Wilbert Siogopi amesema mwaka wa fedha 2021/22 halmashauri hiyo iliidhinishiwa kiasi cha shilingi milioni 150,000,000.

Fedha hizo ni kutoka serikali kuu kwaajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ikiwa ni ujenzi wa jengo kuu, nyumba ya mtumishi na nyumba ya mlinzi.

” Ujenzi umefikia asilimia 85  unatarajiwa kukamilika April 30,2023 na hadi kufikia April 15,2023 jumla ya kiasi cha shilingi milioni 120,000,000 kimeshatumika katika ujenzi huo” amesema mhandisi Siogopi.

Mkuu wa wilaya hiyo akiwa kwenye eneo inapojengwa ofisi ya halmashauri hiyo akapokea taarifa kuhusu ujenzi wa ofisi hiyo ambao tayari halmashauri hiyo imepokea kiasi cha shilingi bilioni 2,750,000,000, tayari ujenzi umefikia asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika Juni 30,2023. 

Taarifa hiyo imesomwa na mkuu wa idara ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu wa wilaya hiyo Shakira Hamisi  kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo.

Amesema ujenzi huo unatekekezwa kwa awamu kulingana na mapokezi ya fedha kuja kwa awamu,mwaka wa fedha 2020/21 halmashauri iliidhinishiwa kiasi cha shilingi milioni 750,000,000 ikiwa ni fedha kutoka serikali kuu kwaajili ya ujenzi wa jengo la ofisi ghorofa moja.

Ofisi hizi tunazijenga kwenye kijiji cha Isenge kata ya Dutwa, awamu ya pili tuliidhinishiwa kiasi cha shilingi bilioni 1,000,000,000 na awamu ya tatu bilioni 1,000,000,000″ amesema Hamisi 

Ujenzi wa jengo la halmashauri hiyo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.8 na utakuwa na vyumba 66 na kumbi mbili za mikutano.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma