skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Wakati Tanzania ikiubainisha mwelekeo wake kuwa wa nchi ya viwanda ambavyo vitazalisha ajira na kuchochea vijana kujiunga na vyuo vya ufundi, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, amewataka viongozi wanaouhusika na ujenzi wa mradi wa ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi nchini kukabidhi jumla ya VETA 29, (25 kwa ngazi ya halmashauri na 4 kwa ngazi ya mkoa ) vyenye thamani ya bilion 48.5 ifikapo May 2022.

Ametoa tamko hilo wakati akiweka jiwe la msingi katika chuo cha VETA chenye ukubwa wa ekari 21 katika  kata ya Nyumbigwa wilayani Kasulu ambacho ni miongoni mwa  vyuo 4 vya Kigoma, Njombe, Geita na Rukwa vilivyokamilika huku vingine 29 vikitakiwa kukamilika mnamo mwezi Juni 2022.

Waziri Ndalichako amezindua jumla ya  majengo 16 yaliyokamilika  kwa awamu ya kwanza yenye thamani ya bilioni 2.197  na majengo 7 ambayo haya jakamilika kwa awamu pili yenye thamani ya 1.2 huku milioni 229.842 zikiwa zimeidhinshwa tayari kwaajili za ununuzi wa samani za uendeshaji wa chuo hicho

Profesa Ndalichako akifungua rasmi chuo cha mafunzo ya ufundi Kasulu mkoani kigoma

Miongoni mwa majengo yaliyokamilika ni pamoja na karakana ya umeme, magari, uwashi na seremala, jengo la utawala, vyumba vya madarasa 2, bwalo, vyoo vya nje 3, na nyumba 2 za walimu huku majengo ambayo hayajakamilika ni pamoja na majengo ya usindikaji,mabweni 2 pamoja na nyumba za walimu.

Amesema lengo la kuwa na vyuo vya ufundi ni kuhakikisha kuwa watoto wanamaliza shule wakiwa na ujuzi, na kwa watoto waliondelea na shule wanakuwa na taaaluma pamoja na utakowasidia kujiajiri ili kuondokana na wimbi la vijana wengi kukosa ajira

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa VETA nchini Pancras Bujulu amesema kuwa mpaka sasa wana wanafunzi 60 waliiomba na kuchaguliwa kujiunga na chuo hicho katika kozi za ufundi magari 22, fundi umeme 22 na ushonaji 16 na kusisitiza kuwa mpaka sasa wanazo computer 20 kwaajili ya kuanza mafunzo ya compute, na pindi mitambo itakapowasili mafunzo yataanza rasmi mnamo January 2022.

Vivyo hivyo ameiomba serikali wilayani kasulu kuwaongeza eneo kwaajili ya ujenzi wa majengo yaliyobaki na upanuzuzi wa majengo kwa matumizi ya baadae.

Naye mkuu wa wilaya ya Kasulu, col Isaac Mwakisu ameipongeza wizara ya elimu nchini na kuahidi kutunza miundombinu iliyojengwa  kwa kuhakikisha inakuwa imara na inadumu kwa muda mrefu bila kuharibiwa kwaajili ya ustawi wa jamii nzima.

Wilaya ya Kasulu sasa inakuwa na jumla ya vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi Vinne (4) ikiwemo FDC Kasulu inayotoa mafunzo ya ufundi, chuo cha ufundi Nyamidaho kilichoanzishwa katika eneo linaloathiriwa na wakimbizi, chuo cha ufundi Dogeza na chuo cha ufundi Kasulu Nyumbigwa.

Mwandishi: Adela Madyane

Mhariri: Prosper Kwigize

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma