Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka…
Na. Herieth Menshi- TPC Tabora
Chuo cha uandishi wa Habari na Utangazaji cha Tabora PolytechnicKinatarajia kutoa vitambulisho kwa wanafunzi wake ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo na kuongeza ujuzi.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa idara ya uandishi wa habari na utangazaji katika chuo hicho Bw. Ibrahim Ally wakati akijibu hoja ya wanachuo kukosa ushirikiano kutoka kwa wadau na wananchi wanapohitaji taarifa mbalimbali.
Bw. Ally amesema kuwa changamoto hiyo wameshaipatia ufumbuzi wa kuanzisha mfumo wakuandaa vitambulisho ambavyo vitatolewa ili kuwatambulisha wanafunzi hao na kuwasaidia wakati wa kukusanya taarifa kwa Uhuru na kuwatoa hofu wananchi pindi wanapotoa taarifa
Amebainisha kuwa mkakati mwingine ni pamoja na wanafunzi kupelekwa katika ziara za mafunzo katika vyombo mbalimbali vya habari ndani nan je ya mkoa wa Tabora ili kujifunza zaidi
Hatua hizo za chuo zinakuja kufuatia wanafunzi wanaosomea fani yauandishi wa habari na utangazaji katika chuo hicho kilichopo mkoani Tabora kulalamikia changamoto wanayokutananayo ya kukosa ushirikiano wanapohitaji taarifa katika jamii inayowazunguka.

Akizungumza na Buha FM, mmoja wa mwanafunzi wa tasnia hiyo Paulina Majaliwa amesema changamoto kubwa inayopelekea kutokuwasilisha taarifa kwa wakati ni kutokuwepo kwa ushirikiano baina ya watoa taarifa.
“changamoto ni nyingi ni kukosa ushirikiano kwa watoataarifa ambao tunawafikia kuchukua taarifa.”amesemaPaulina majaliwa
Kwa upande wake Esperance Ramadhani ambae pia ni mwanafunzi wa ngazi ya stashaahada amesema wananchi hawapotayari kutoa taarifa zilizopo katika jamii kutokana na uoga wa kuhojiwa na kutoa taarifa zinazowakabili katika jamii na kuhofia sauti zao zinapelekwa wapi kwani suala Hilo linatokana na nadharia potofu na hupelekea kutokupata taarifa
Baadhi ya wananchi wakazi wa mjini Tabora wamesema kuwa sababu zinazopelekea watu wengi kukataa kuhojiwa na kupigwa picha ni kutokana na taarifa anayohitaka mwandishi kuhusisha kuikosoa serikali hivyo wanahofia kufuatiliwa na viongozi