skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini ambae pia ni Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amegawa cherehani 100 kwa wanakikundi 362 kwa lengo la kuanzisha kiwanda cha ushonaji na kujikwamua kiuchumi.

Cherehani hizo zenye thamani ya shilingi milioni 30 zimegawiwa kwa vikundi 25 huku kila kikundi kikipokea cherehani 4 kutoka katika kata tofauti wilayani Kasulu.

Akigawa cherehani hizo, mbunge Ndalichako amesema cherehani hizo zimepatikana kutokana na mahusiano mazuri yanayotengenezwa na Rais Samia Suluhu Hassan na nchi nyingine kisera na kijamii kwaajili ya maendeleo ya nchi hizo.

“Tumepata cherehani hizi kwa ufadhili wa China, ninamshukuru Balozi wa China nchini Tanzania kAwa ushirikiano wake wa kuwawezesha wananchi wa Kasulu kiuchumi
kwa kutimiza hitaji la upatikanaji cherehani”Amesema Ndalichako

Ameeleza zaidi kuwa wanachi waliopata cherehani hizo wahakikishe wanazitumia vizuri na kuongeza ufanisi kwa lengo la kupata mafanikio kiuchumi.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamii halmashauri ya Kasulu Mji Dollar Kusenge amemshukuru Mbunge kwa kutoa cherehani kwani zimepunguza mzigo ambao halmashauri ingepaswa kuubeba kupitia pesa za asilimia 10 kwa vijana na akina mama.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Kasulu mji Noel Hanura amesema anafurahishwa na uongozi wa mbunge Joyce Ndlichako kwani ni shirikishi kwa wananchi na kuwataka wananchi kuthamini mchango wake na kuhakikisha wanatunza vitendea kazi hivyo kwa kufanya kazi iliyo kusudiwa.

Venancy Msole ni Mlezi wa vikundi vya vijana (VIJARUNGU) kutoka kata ya msambala, ameseema cherehani hizo zimejibu ndoto za vijana hao kwani vijana wanayo fani ya ushaonaji na kilichokuwa kimebaki ni vitendea kazi ambavyo vimepatikana leo hii.

Naye Letisia Nzozi katibu wa wazee halmshauri ya wilaya ya Kasulu amesema kuwa akina mama hawatavaa tena nguo zilizochanika, na kwamba watahakikisha wanafanya kazi kwaajili ya kujiongezea kipato na kumtia moyo mbunge wao kwa kazi nzuri anayofanya kwa wananchi wake.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma