skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Mwandishi wetu, Kigoma

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA leo kimezindua Operesheni maalumu ya kudai katiba mpya ya Tanzania kama sehemu ya kuwa na ulingo sawa wa siasa kwa ajili ya maendeleo ya taifa hilo

Uzinduzi huo umefanywa na viongozi wote wa chama hicho taifa, kanda na mkoa wa Kigoma katika viwanja vya Mwanga mjini Kigoma, ambapo mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesisitiza kuwa taifa hilo linahitaji Katiba mpya

Moja ya mambo yanayotajwa kusukuma madai ya Katiba ni kuzorota kwa huduma za jamii, wananchi kunyimwa haki mbalimbali ikiwemo wanawake kukandamizwa na sheria zilizopo hususani kodi na ushuru wa biashara, viongozi wa baraza la wanawake la chama hicho Catherine Ruge na Sharifa Suleiman kabla ya mkutano huo walitembelea Soko la Nazareth mjini Kigoma ambalo ni maarufu kwa wanawake wajasiriamali na kukutana na malalamiko ya tozo za ushuru zinazotajwa kutozingatia maslahi ya wanawake na mitaji yao

Mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema mkoa wa Kigoma Bw. Boniphace Chuzura ameeleza kuwa serikali ya CCM imeshindwa kushughulikia matatizo ya kaya masikini kupitia TASAF kwa kuwatumikisha kutengeneza barabara za mitaa kazi ambayo inapaswa kufanywa na TARURA

Suala la muungano nalo ni ajenda ya CHADEMA ambapo naibu Katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalimu anataja kuwa muungano una thamani lakini kuna kasoro nyingi, ikiwemo kutokuwepo na serikali ya Tanganyika

“Nitakuwa wa mwisho kusema muungano haufai au kushabikia uvunjike, lakini hoja yetu CHADEMA ni pande zote zinazounda muungano zitambulike ikiwemo serikali ya Tanganyika” anasisitiza Salumu Mwalimu

Kuhusu mwelekeo wa serikali ya Dr. Samia Suluhu Hassan kuonesha nia ya kufufua mchakato wa katiba Mpya, katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika anatilia shaka utayari huo akihoji kuhusu bajeti na mabadiliko ya sharia

MnyikaKuhusu masuala ya uraia pacha kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ambao wanalalamikia kukosa haki za utanzania baada ya kuchukua uraia katika nchi wanazoishi, makamu mwenyekiti wa CHADEMA Antipas Tundulisu anasema mwarobaini wake ni katiba mpya

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa maeneo yaliyowahi kuwa ngome ya chadema kabla ya mvuto wake kunyauka na kuchukuliwa na ACT wazalendo na baadaye CCM kutwaa majimbo yote na kata zote katika uchaguzi wa maka 2020

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma