skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Adela Madyane- Kigoma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema wanaendelea kuisimamia serikali ili kuhakikisha wanafikia mwisho wa mambo ya uwekezaji wa bandari  ili kuanza utekelezaji utakaoleta matokeo chanya kwa wananchi.

Amesema kwa sasa chama kinatoa maelekezo kwa serikali kuongeza msukumo wa kushirikiana na sekta binafsi katika kujenga na kuendeleza uchumi wa nchi.

” Msimamo wa chama ni kuisimamia serikali ili kutekeleza ilani ya chama, ibara ya 22 inatutaka kuielekeza serikali kuweka msukumo na kipaumbele cha kushirikiana sekta binafsi katika kushirikiana, kuendeleza na kujenga uchumi wa nchi na ibara ya 59 inatoa maelekezo kwa meneo mahususi ya uwekezaji na uongezaji wa tija nchini, tunashukuru serikali imeanza kuongeza tija kwenye eneo la bandari” Amesema Chongolo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wananchi wa mkoa wa Kigoma kwa pamoja na wananchi wa mkoa wa Katavi katika Uwanja wa Kituo cha Maendeleo Mwanga mjini Kigoma jana

Amesema wanufaika wa matokeo ya uwekezaji ni wa Tanzania hivyo hawatakaa kimya wala kuyumbishwa katika kuzifikia fursa zinazojitokeza kwa lengo la kuendeleza nchi.

Amesema chama hakipo tayari kuona fursa ya uwekezaji wa bandari inachukuliwa na nchi nyingine za jirani kwani kwa kufanya hivyo itakuwa ni kiwaumiza wananchi wenye hamu na nia ya dhati ya kufanya maendeleo 

“Lazima tukimbilie fursa, tusiwaachie majirani zetu, tukikaa kienyeji mambo yetu yataharibika, serikali ipo timamu na inaamua kwa maslahi mapana ya nchi, tumeagiza serikali kuleta matokeo chanya na si vinginevyo” amesisitiza Chongolo 

Umati wa wanaCCM na wanachi wengine kutoka mikoa ya Katavi na Kigoma wakisikiliza maelezo ya viongozi wa CCM na serikali kuhusu uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam utakaofanywa na kampuni ya DP World kutoka Dubai

Akifafanua zaidi Atupele  Mwakibete naibu waziri wa uchukuzi amesema uwekezaji wa bandari utasaidia kuitunza nchi ya Congo DR ambayo ndio inaongoza kwa kusafirisha mizigo kwa kusafirisha tani milioni tatu za mzigo kwa mwaka ikifuatiwa na nchi ya Zambia na Rwanda kwa tani milioni moja kwa mwaka na kisha Malawi tani laki sita na Uganda tani laki moja.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma