Waandishi wa habari wa Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma wametakiwa kutumia Takwimu za sensa…
Na ZAKIA NDULUTE – Kibondo
Chama cha Mapinduzi kimewataka wazazi nchini kuhakikisha Watoto wao wanapata malezi mazuri sambamba na kuhudhuria masomo shuleni ili kudhibiti mmomonyoko wa maadili na kuondokana na wimbi kubwa la watototo mitaani
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya kibondo Comrade Hamisi Tahilo wakati wa ufunguzi wa wiki ya jumuiya ya wazazi iliyofanyika katika kata ya Mabamba wilayani Kibondo
Tahilo ameongeza kuwa suala la malezi hafifu limechangia utoro sugu wa watoto na wengi kutoripoti shuleni kwa wakati hali inayohatarisha ustawi wa jamii nchini
Ametoa wito kwa jumuiya ya wazazi kuitumia wiki ya wazazi kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuzingatia malezi bora ya familia hususani Watoto na kuhakikisha taifa linakuwa na raia wema

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm mkoa wa Kigoma Mh. Jamali Abdallah Tamimu ambaye alihudhuria sherehe hizo kama mkazi wa Mabamba alitumia nafasi ya kusalimu wananchama kwa kuweka bayana kuwa chama cha mapinduzi kimekuwa cha mfano Afrika kutokana na umahili na umalidadi wake wa kujali maadili na kuwataka wadau wa chama hicho kuendelea kuwa na ushirikiano mzuri kwa viongozi wao katika kuongeza juhudi za kuleta maendeleo bora ya wananchi
Naye mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya kibondo Ndugu Phales Nzobhona alisema kuwa jumuiya ya wazazi imepata mafanikio makubwa ambapo idadi imeongezeka kutoka wanachama 6580 hadi kufikia idadi ya wanachama 6602 ambapo wanawake ni 2960 na wanaume ni 3620 pamoja na wanachama wapya 22 ambao wote ni mchanganyiko
Aidha kwa upande wake katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya kibondo Ndugu Evarist Msafiri amekemea vitendo viovu vya ukatili kwa watoto na kuwahimiza wazazi kuwa na ushirikano mzuri kwa kuvikemea na kuviripoti pindi vinapotokea katika maeneo yao
Kila mwaka mwezi APRILI hufanyika maadhimisho ya wiki ya jumuiya ya wazazi na kauli mbiu ya mwaka huu ni TAIFA BORA NI KUTOKANA NA MALEZI BORA YA WATOTO ‘