skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Raia wa Burundi wanaohifadhiwa katika kambi za Wakimbizi wilayani Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma nchini Tanzania, wamesema wapo Tayari kurejea Nchini Burundi, endapo serikali ya Burundi itawahakikishia usslama kwa kudhibiti matukio ya uharifu, chuki za kisiasa, migogoro ya ardhi na kifamilia.

Wawakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara inayoendelea wilayani Kibondo na Kasulu wakimbizi hao ambao wengi wao wamekimbia kwa zaidi ya awamu moja, wamemweleza Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Burundi, Calinie Ndabarushimana aliyeambatana na viongozi wengine katika kambi za Nyarugusu na Nduta mkoani Kigoma kwa lengo la kuhamasiaha ndugu zao kurejea nchini mwao.

Fredirick Ntakizimana ni mmoja kati ya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu waliopata nafasi ya kutoa ya moyoni kuhusu hamasa ya kurejea nchini mwao na taarifa walizonazoo kuhusu usalama wa nchi yao

Hakuna mtu anaweza kukataa kurudi nyumbani, vituu tulivyoacha Burundi ni vingi na vyenye thamani ukilinganisha na tulivyonavyo hapa Kambini, Maisha tunayoishi katika kambi siyo mazuri, lakiini hatuna uhakika na usalama nchin mwetualisisitiza Ntakizimana.

Idadi ndogo ya wakimbizi wa Burundi imekuwa ikijiandikisha kwa hiyarii kurejeshwa nchini mwao chini ya utaratibu wa UNHCR, na serikali za Burundi na Tanzania ambapo pia hupewa misaada mbalimbali ikiwemo fedha taslimu kuwawezesha Kwenda kuanza Maisha upya. Hata hivyo Kassun Pacal anasema wanaojiandaikisha kurejea wanafanya hivyo kutokana na mbinyo wa huduma ndani ya kambi

Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Burundi Calinie Ndabarushimana akicheza na watoto wakimbizi wa Burundi katika Kambi ya Nduta wilayani Kibondo mkoani Kigoma mapema leo walipowasili katika ofisi za idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani katika kambi hiyo.

Baada ya kupokea maoni ya wakimbizi hao pamoja na wengine Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Burundi Calinie Ndabarushimana amewatoa hofu wakimbizi kuwa Burundi ina amani na usalama wa kutosha na hakuna sababu ya raia wake waishio uhamishoni kuogopa kurejea.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Izack Mwakisu ameweka msisitiza wa serikalii ya Tanzania akiweka bayana kuwa wakimbizi hawanabudi kurudi kwao

Mkurugenzi idara ya Wakimbizi Wizara ya mambo ya ndani nchini Tanzania Sudi Mwakibasi ameeleza kuwa wakimbizi wanaendelea kujiandikisha na waweze kurejea nchi mwao na kwamba zaidi ya wakimbizi 3000 tayari wamejiandikisha.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwaka mmoja kwa serikalii ya Burundi kuwatuma viongozi wake kutoka wizara ya mambo ya ndani kuzuru kambi za wakimbizi kuhamasiaha raia wake kurejea nchini mwao

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwaka mmoja kwa serikalii ya Burundi kuwatuma viongozi wake kutoka wizara ya mambo ya ndani kuzuru kambi za wakimbizi kuhamasiaha raia wake kurejea nchini mwao

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma