Na. Irene Bwire -PMO na Anita Balingilaki Buha - Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka…
Matinde Nestory, Mwanza
Wakala Wa Usajili Wa Biashara na Leseni (BRELA),imewataka wamiliki waliosajili makampuni kuwasilisha taarifa za mmiliki manufaa kabla ya June 30 mwaka huu.
Rai hiyo imetolewa na kaimu Mkuu wa sehemu ya makampuni (BRELA) Bi Leticia Zavu wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa chuo Cha Bank Kuu jijini Mwanza na kusema kuwa taarifa za kuwasilisha mmiliki manufaa zinapaswa kuwasilishwa ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa Sheria ili kupata taarifa sahihi za mmiliki halali wa kampuni.
Bi Zavu ameongeza kuwa taarifa hizi ni muhimu kwa nchi na inaleta manufaa na msajili kujua mmiliki halali wa hisa katika kufanya biashara.
“Mmiliki manufaa ni mtu ambaye anamiliki hisa kuanzia 5% na kuendelea inaweza ikawa ni hisa au Ile Mamlaka aliyekuwa nayo ndani ya kampuni katika kufanya na Kutoa maamuzi ya kuteua wakurugenzi na kufanya maamuzi mbalimbali yanayohusiana na kampuni” amesisitiza Bi zavu
Ameeleza kuwa taarifa za Mmiliki Manufaa pia zitawezesha kumfahamu mtoa maamuzi katika kampuni kwa lengo la kupunguza mianya ya utakatishaji fedha na kutambua vyanzo vya fedha za wamiliki wa makampuni kwa usalama wa Taifa na uchumi kwa Ujumla.
“lazima ifahamike kwa wadau na wamiliki wa makampuni kwani inatoa wigo kwa Serikali kufanya maamuzi sahihi ya kuzuia masuala ya utakatishaji fedha,rushwa,kupanga kodi,pamoja na kuzuia mianya ya ugaidi”amesema Bi Zavu.
Sanjari na hayo ameongeza kuwa awali mfumo ulikuwa unapokea taarifa bila kujali kinachofanyika,hivyo suala hili likawa chanzo cha mianya ya rushwa na tishio la kiusalama, ndiyo maana Sheria ya kuzuia utakatishaji fedha ikapitishwa, hivyo kampuni zinatakiwa kuwasilisha taarifa za Wamiliki Manufaa ili ifahamike chanzo cha fedha wanazomiliki.
Kwa upande wake Afisa usajili Jacob Mkuye amesema kuwa wadau wa biashara,mawakili na makampuni lengo likiwa ni kuwakumbusha wajibu wa kuwasilisha taarifa za mmiliki manufaa.
Nae Afisa Sheria( BRELA) Vicensia Fuko amesema kuwa taarifa za mmiliki manufaa zinatakiwa kuwasilishwa kwa msajili wa makampuni BRELA kutokana na mabadiliko ya Sheria yaliyofanyika mwaka 2020 ikiwa na lengo la kuongeza uwajibikaji katika makampuni pamoja na kupambana na uharifu wa kifedha.
“Tunasimamia matakwa ya Sheria kuhakikisha taarifa zinawasilishwa BRELA na kila kampuni pamoja na hilo tumegundua Kuna changamoto katika ujazaji wa taarifa”amesema Bi Fuko.
Kwa upande wake Wakili Salehe Nassor amesema kuwa BRELA inahitaji taarifa sahihi za wamiliki wa kampuni na kusikuwepo na mkwamo wa kuwasilisha taarifa
Hata hivyo ameitaka BRELA kuendelea kutoa elimu ambayo itawasaidia wamiliki wa kampuni kujua sheria na taratibu za mmiliki wa hisa.