skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Habari za hivi punde kutoka Goma mashariki mwa DRC zinataja kuwa kikundi cha waandamanaji wamevamia na kuharibu vibaya moja ya kambi ya askari wa Umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MUNOSCO)

Tukio hilo ambalo ni mwendelezoo wa maandamano yaliyoanza jana, limetokea majira ya saa 12 alfajiri wakati vijana hao walipovamia na kufanya uharibifu mkubwa ikiwemo uporaji.

Mwandishi wa Buha FM aliyeko Goma anataarifu kuwa, vijana hao wenye msimamo mkali lengo lao ni kufukuza vikosi vya kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa nchini Congo MONUSCO vilivyoweka kambi katika maeneo kadhaa ya Goma mji mkuu wa mkoa wa Kivu ya Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

Waandamanaji waliovamia kambi ya pili ya kikosi cha Umoja wa mataifa cha kulinda amani nchi DRC wakipora mali za MUNOSCO katika mji wa GOMA

Tanzama video ushuhudie kadhia hiyo ya waandamanaji dhidi ya majeshi ya Umoja wa mataifa

Waandamanaji hao wamevamia makao mengine ya MUNOSCO yaliyoko eneo liitwalo TMK ambapo vijana wakiingia ndani na kupora vitu mbalimbali hususani Vitanda, Magodoro na samani nyingine za ndani.

Wafanya kazi wengi wa Monusco waliondoshwa kwa njia ya Helikopta usiku wakuhamkia Leo hii kwakuhofia maisha yao. Wengi wao walisafirishwa hadi mjini Kinshasa mji mkuu wa DRC kutokana na hali ya wasiwasi iliyo shuhudiwa tarehe July 25.

Leo Siku ya pili mfululizo ya maandamano ya Raia wanaotaja kuchukizwa na kuendelea kuwepo kwa machafuko na vita huku vikosi vya kulinda amani vikishuhudia bila vikosii vya UN kuchukua hatua dhidi ya makundi ya waasi.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma