skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki – Simiyu

Waziri wa maji Jumaa Aweso amesema kuwa mradi wa maji wa ziwa Viktoria ambao unatarajiwa kuanza kutekelezwa Julai 2023 na utatekeelezwa kwa wakati mmoja kwenye wilaya zote za mkoa Simiyu lengo likiwa kuwawezesha wananchi wa mkoa huo kupata huduma ya maji safi na salama.

Waziri Aweso ameyasema hayo mjini Bariadi wakati wa utiaji saini ya kuanza kwa ujenzi wa mradi huo utakaotekelezwa na kampuni kutoka nchini China ambapo amesema mradi huo utawezesha upatikanaji wa maji kwa wananchi, mifugo na shughuli za umwagiliaji mkoani humo.

Aidha Waziri Aweso amesema kuwa itaanzishwa mamlaka kubwa ya maji Simiyu ambayo itahusika na usimamizi wa mradi huo huku akimteuwa aliyekuwa Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mijini na Vijijini (RUWASA) mkoa wa Simiyu, mhandisi Mariam Majala kuwa mkurugenzi wa mamlaka ya maji Simiyu (SIBUWASA) na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Mjini Bariadi (BARUWASA) Mhandisi Musalika Masatu kuwa meneja ufundi wa mamlaka hiyo.

Waziri wa maji JUma Aweso akihutubia wakazi wa Bariadi mkoani Simiyu

Awali katibu mkuu wa wizara hiyo mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema mkataba uliosainia leo ni wa bilioni 166.8 kati ya fedha hizo zipo bilioni 440 za utekelezaji wa maji kutoka ziwa Victoria na ujenzi utafanywa na kampuni kutoka nchini China na utaanza mwezi Julai.

Awali mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda amesema mradi huo unatarajiwa kuwanufausha jumla ya kata 26 vijiji 103 na wakazi zaidi ya laki nne.

Mbunge Mashimba Ndaki akitoa shukurani kwa serikali na kuhimiza maji yawe kwa binadamu na mifugo

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki amewaomba watekelezaji wa mradi huo kutosahau eneo la kunyweshea mifugo huku mbunge wa viti maalum kupitia vijana Lucy Sabu akisema mkoa huo ulikuwa na changamoto kubwa ya maji.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma