skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Teresia Mande – Singida

Shirikisho la wachimba madini Tanzania FEMATA limedhamiria kuanzisha Bank ya wachimba madini nchini ili kuondokana na changamoto ya mitaji inayowafanya washindwe kuendelea katika kazi zao.

Wakizungumza baada ya kikao cha kamati tendaji ya shirikisho hilo kilichofanyika mjini Singida baadhi ya wajumbe wamesema uanzishwaji wa bank utasaidia kupata mikopo kwa urahisi.

Adhima hiyo ya uanzishwaji wa bank ni moja ya maazimio yaliyotokana na kongamano la wiki ya madini iliyofanyika jijini Mwanza pamoja na marekebisho ya katiba ya FEMATA ili iendane na wakati.

Aidha rais wa FEMATA John Bina amesema ili shirikisho hilo liwe imara zaidi ni lazima kufanya marekebisho ya katiba ili iwafae kwa wakati wa sasa na wakati ujao na kutimiza malengo yao ya kuanzisha bank.

Naye kaimu afisa madini mkazi Mkoa wa Singida Chone Malembo aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao hicho amesema jambo la uanzishwaji wa bank ya wachimbaji limeungwa mkono na wachimbaji wengi hivyo ni vizuri kuweka mikakati bora ya uanzishwaji wa bank hiyo.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma