Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Na. Matinde Nestory, Mwanza
Vijana mkoani Mwanza wametakiwa kujitambua na kutafuta ajira zilizopo duniani, ikiwemo kujiajiri wenyewe kwa kutumia fursa za kibenk ambazo zitawakwamua kiuchumi na kujipatia kipato.
hayo yalibainishwa wiki hii na Mkuu wa chuo Cha benk Kuu Dr Nicas Yabu wakati akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo vya IFM, SAUT, BANK KUU ACADEMY, CBE pamoja na wajasiliamali wadogo wadogo katika maadhimisho ya Miaka 56 ya benk Kuu Tanzania yaliyofanyika Katika ukumbi wa benk Kuu jijini Mwanza.
Akizungumzia mafanikio amesema, mfumo wa malipokatika sekta za kibenki umeimalika, ambao ni pamoja na usambazaji wa sarafu kuifikia nchi nzima,

Aidha Bank Kuu imefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei kuwa talakimu moja (single digits) yenye 4% pamoja na sarafu iko imara kulingana na sarafu nyingine.
“Vijana ni lazima muwe na nidhamu na Kaz, kujiajiri Katika sekta ya fedha ili muweze kujikwamua Katika wimbi la kukosa ajira tumieni ujuzi na maarifa mliyoyapata vyuoni ili muweze kusaidia jamii na taifa kwa ujumla” alisema Dr Yabu.
Kwa upande wake mtaalamu wa rasilimali watu Siophoro Kishimbo alisema kuwa Vijana wamejengewa uwezo namna ya kuingia katika soko la ajira na jinsi gani waweze kujiamini pamoja na namna ya kuandika wasifu ambao utawasaidia kupata ajira duniani.
“Tumetumia fursa hii ili tuweze kuwajengea namna ya kujiamini wanapoingia kwenye usaili na vitu gani wanatakiwa wafanye na vitu gani wanatakiwa kuepuka” Amesema Kishimbo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vya IFM na SAUT wamesema kuwa Elimu waliyoipata itawasaidia kuwaongezea maarifa pamoja na ujuzi na kuwafanya kuajirika kirahisi.