skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Mkuu wa Wilaya ya Nyamaga Bi Amina Makilagi amekabidhiwa msaada wa madawati yenye thamani ya shilingi  milioni 65,000,000  na The  desk and chair foundation Mkoani Mwanza kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondary zilizopo Mkoani hapa.

 Bi makilagi amepokea msaada huo wa madawati may 27 mwaka huu katika uwanja wa Grand hall uliopo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza na kusema kuwa madawati hayo yatawasaidia wanafunzi wa Mkoa wa Mwanza katika kusoma na kukuza taaluma ya kielimu na kuwajengea uwezo wa kupanuka kiakili na kimtazamo.

“Mkoa wa Mwanza tunahitaji zaidi ya madawati 265 kwa shule Zetu za msingi na sekondary  ambapo tumepokea shilingi bilion 1.69 ambazo zinakwenda kujenga madarasa ya kawaida 39 na madarasa ya ghorofa  64 ambayo madarasa yote hayo yakikamilika yatahitaji madawati” amesema Bi Makilagi.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Amina Mkilangi akipokea msaada wa viti na madawati kutoka kwa viongozi wa taasisi ya Desk and Chair Foundation

Ameongeza the desk and chair foundation imewasaidia msaada huo wa madawati ambao utasaidia mahitaji ya wanafunzi wa sekondary na shule za msingi  katika Mkoa wa Mwanza na kuwataka wadhamini hao kuendelea kujitokeza kutoa msaada katika Sekta mbalimbali nchini Tanzania.

Nae  Mkurugenzi Mwakilishi Tanzania The desk and chair foundation yenye makao makuu nchini uingereza Sibtain Meghjee amesema kuwa madawati 455 na meza18 na viti 108 kwa ajili ya shule za chekechea (563) iliyopo katika Kijiji Cha malela Mkoani Singida na mantale na kila meza ya duara itachukua wanafunzi sita,pamoja na madawati 355 ni kwa ajili ya wanafunzi wa Mkoa wa Mwanza.

Aidha ametaja miradi inayoendelea  kuwa ni ujenzi wa vyoo 20 katika shule ya kilimani Wilaya Ilemela,mradi wa maji wa kuboresha kisima katika zahanati iliyopo Mkoani Simiyu na miradi iliyokamilika ni pamoja na mradi wa kusukuma maji katika hospitali ya Bukumbi inayomilikiwa na kanisa catholic, mradi wa kufadhili magodoro 1000 kwenye Gereza kuu la  Butimba,mradi wa kufikisha maji kwenye makazi ya wazee Bukumbi, uchimbaji wa kisima kirefu kwenye gereza la Butimba pamoja na  mradi wa kugawa vyehehani 200.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyamaga Biku kotecha amesema kuwa msaada huo wa madawati utawasaidia wanafunzi katika Elimu Yao ambayo ni ufunguo wa Maisha.

Hata hivyo amempongeza the desk and chair foundation kwa msaada huo ambao umekua Chachu ya mafanikio katika Mkoa wa Mwanza na kuomba wafadhili  mbali mbali wajitokeze kutoa msaada madawati  katika shule za msingi na sekondary ili kuweza kufikia malengo yaliyopangwa na serikali awamu ya sita ya kila mwanafunzi akae juu ya dawati.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma