skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Felister Nestory- Mwanza

Mganga Mkuu wa jiji  Mwanza daktari Pima Sebastian amewataka wananchi kujitokeza katika kuchangia damu salama  ili kusaidia kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na wagonjwa na wagonjwa wengine wanaohitaji kuongezwa damu.

Dr. Pima amesema hayo katika eneo la Kijijin bar jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa maonyesho yanayosafiri ambayo yamekutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa  ambayo umeanza  Mei 12 hadi Mei 15 mwaka huu.

Amesema kuwa ni muhimu wananchi kujitokeza katika zoezi la kuchangia damu hali ambayo itapelekea kupungua kwa vifo vitokanavyo na upungufu wa damu katika bank ya damu.

Dr. Pima Sebastian, Mganga mkuu wa jiji la Mwanza akihamasishwa jamii kuchangia damu

“Sisi ndani ya jiji tuna malengo ya kukusanya unit za damu takribani 200-250 ndani ya mwezi mmoja na tunafahamu wote ndani ya jiji sisi tunazo hospitali kubwa ikiwemo hospital ya Kanda  Bugando lakini na hospitali nyingi bazo zinafanya huduma za dharura za Amina mama wajawazito ambao wengi wao uhitaji damu” amesema Dr Sebastian.

Hata hivyo ameongeza kuwa sababu ya vifo vitokanavyo na uzazi ni pamoja na akina mama wajawazito kutoka damu kabla wakati au baada ya kujifungua hali ambayo inatishia maisha ya akina mama.

Zoezi hili kwetu sisi ni  muhimu lengo lake ni kuokoa maisha na wadau mbalimbali wamekua wakishiriki ikiwemo kituo chetu Cha Kanda Cha damu salama,hospitali ya wilaya ya Nyamagana, hospital ya Mkoa ya sekouture na kituo Cha damu salama hospitali ya rufaa ya Bugando wadau wote hao tunahakikisha uwepi wa damu ndani ya jiji ni ya kutosheleza” amesema Dr Sebastian.

Nae  Deborah Kihedu muuguzi kutoka damu salama Kanda amesema kuwa jamii inatakiwa ifahamu kuwa ukichsngia damu umeokoa maisha ya mamia ya wagonjwa.

Pia ameongeza kuwa mchangiaji wa damu damu anatakiwa awe mwenye uzito wa kilo 50 na kuendelea, kupima wingi wa damu 12.5 na kuendelea,kuonana na mshauri ambaye atamwambia Kama amekidhi vigezo vyote vya kuchangia damu,mfuko wa damu wenye namba maalum na kuchangia damu yenye ujazo wa millimetre 450.

Kwa upande wake Judith Divanji Mzurikwao mjasiliamali  na muandaaji wa  matamasha na maonyesho yanayosafiri  amesema kuwa amekuwa jamii ikihamasihwa kuchangia  damu salama hii itasaidia kupunguza uhaba wa damu katika bank ya damu.

Hata hivyo ameitaka jamii iachane na Mila potofu kwamba ukitoa damu  utakiwi kuacha pamoja na kichwa kuuma  Mara kwa Mara hii ni dhana potofu ambayo Haina mashiko.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma