skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Habari na Ananias J.Khalula.

Wazee Halmashauri ya mji wa Kasulu Mkoa wa Kigoma wamepongeza Shirika la OHIDE kuanzisha kituo cha Radio Buha Fm wakielezea kuwa Radio itachochoea uwajibikaji na utatuzi wa changamoto zinazowakumba kama vile upatikanaji wa huduma za kijamii, matibabu bure kwenye vituo vyote vya afya vya mji huo.

Daudi Chitabila ni mzee mwenye umri  (85) mzaliwa wa Kasulu Kata ya Buhoro Kijiji cha Chanza, amesema kiafya anasumbuliwa na tatizo la meno kwa kipindi cha mwaka mzima amezunguka vituo vya afya mbali mbali Halmashauri ya Mji wa Kasulu akiwa na kitamburisho chake cha uzee ila hata siku moja hajawahi  kusaidiwa kupata utatuzi wa kudumu Zaidi ya dawa za  kutuliza maumivu pekee

Mzee Daud Chitabila, mkazi wa wilaya ya Kasulu ni miongoni mwa wazee wanaohimiza uwajibikaji

Chitabila anadai kuwa wazee wengi wanakosa huduma za afya kutokana na baadhi ya watoa huduma kudai cheti cha Bima ya afya na kutotambua kitambulisho cha uzee.

Naye Bi,Grace Kababaye ni mzee mwenye mri (60) mkazi wa kasulu mjini, amesema anasumbuliwa na ugonjwa wa pressure na miguu kwa kipindi cha miaka mitatu hawezi kusimama na kutembea kwa muda mrefu na amekuwa akienda zahanati na vituo vya afya kwa ajili ya kutafuta matibabu ila mara nyingi alichoambulia ni kunyanyapaliwa na wahudumu wa afya.

Kwa mjibu wa Bw, Peter Janga Daktari Mkuu wa Halmashauri hii ya mji wa kasulu mkoa Kigoma, akizungumza na Buha FM, amesema  takwimu za wazee kiserikali kwa miezi mitatu iliyopita kuanzia mwezi julai mwaka huu, wazee kuanzia miaka 60 na kuendela idadi ilikuwa ni Zaidi ya 10,000 na waliyopata vitamburisho vya msamaha wa huduma za kiafya katika hospitali, zahanati na  vituo vya afya ni 8,000 pekee na kwamba wengine wanaendelea kutengenezewa vitambulisho vyao.

Dr. Peter Janga mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu- Akitsoma takwimu za wazee waliohudumiwa

Aidha Dr.Janga amesema kuwa katika kipindi hiki cha UVIKO 19 Halmashauri ya mji huu kupitia Idara ya Afya wamefanikiwa kuwapatia wazee wote huduma ya chanjo na matibabu mengine kwa wakati  kulingana na magonjwa ya uzeeni

Buha Fm imetembelea kaya mbali mbali kwenye mji huo kwa ajili ya kujionea hali halisi ya afya ya wazee ambapo imezungumza na baadhi ya wazee, wengi wakipongeza shirika la OHIDE kuanzisha kituo cha Radio kitakachosaidia kupaza sauti za wazee ili ziweze kusikilizwa na mamlaka.

Sambamba na hayo Bi,Elizabeth Mwandesile, ambaye ni mkazi wa kata ya Mwilamvya Kasulu ameomba Mashirika ya kutetea haki za Binadamu na Serikali kwa ujumla kutumia kituo cha Buha fm katika kutoa Elimu juu ya maswala ya uzee ili vijana kwenye jamii waweze kuwatunza wazee wao pale wanapoanza kuzeeka kwasababu baadhi ya vijana huwapuuza wazazi wao na kupelekea wengi wao kupoteza Maisha kwa kukosa matunzo imara.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma