skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Adela Madyane – Kigoma

WANANCHI wa kata ya Kidahwe katika halmashauri ya wilaya ya kigoma wamechangishana kiasi cha sh 10,000 na matofari 10 kwa kila kaya kwaajili ya kuanzisha ujenzi wa kituo cha afya ili kuondokana na adha ya kutembea kwa zaidi ya kilometa 30 kufuata huduma katika kituo cha afya cha Bitale

Kata hiyo yenye jumla ya wakazi 21000 wamesema ukosefu wa kituo cha afya katika kata yao imechangia wajawazito na wagonjwa wa dharura kulazimika kuingia gharama ya zaidi ya shilingi elfu 50,000 kukodi usafiri huku gharama za kawaida za usafiri zikiwa ni kiasi cha shilingi elfu 7000 jambo ambalo linawaumiza kiuchumi hasa wananchi wenye kipato cha chini

Hayo yamesemwa na Zainab Hamis mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) katani hapo wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho na kusema kuwa zahanati iliyopo ni ndogo ukilinganisha na wingi wa watu jambo linalofanya baadhi ya wajawazito kujifungua nje ya zahanati na wengine kuamua kujifungulia nyumbani

Tunaye datkari mmoja tu na manesi wawili, huduma iliyopo haikidhi mahitaji ya wananchi, wajawazito wanateseka, watu wakipata ajali wanateseka namna ya kupata huduma haraka , na kuna wakati wazazi wanajifungulia ndani ya gari wakati tunawapeleke Bitale au nje na watoto wanapoteza maisha kwa kukosa msaada” amesema Hamis

Wananchi wa kata ya Kidahwe wakichimba visiki na kufyeka kwaajili ya kuandaa eneo la ujenzi wa kituo cha afya

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Kidahwe Simon Musa alisema wameamua kuanzisha ujenzi ili kuhakikisha wanapata huduma ya karibu na kuondoa changamoto hiyo ambayo inaathiri zaidi wajawazito na watoto

Kwa upande wa diwani wa kata hiyo Heri Kigufa amesema serikali ya kijiji imetoa zaidi ya ekari 25 kwaajili ya ujenzi huo na kwamba hatua za awali za ujenzi zinaendelea ikiwemo kufyeka na kutoa visiki

Amesema mpaka sasa akaunti ya ujenzi ina zaidi ya sh. milioni 1.6 na ahadi kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo shule ya sekondari ya Mikamba walioahidi kutoa tripu 20 za mawe

“Tutahakikisha tunafikia asilimia 20 kabla ya mwezi Julai ili tuanze ujenzi wa OPD haraka ikiwa ni kufungua njia kwa serikali kuendelea na ujenzi wa majengo yaliyobaki, nawashukuru sana wananchi kwa kujitoa na kuhakikisha tunafanikisha hili” Alisema Kigufa

Naye Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Assa Makanika ameahidi kutoa kiasi cha sh milioni tano kutoka mfuko wa jimbo itakayo ingia kwenye akaunti ya ujenzi ya wananchi ili kufikia asilimia 20 ya pesa za wananchi zinafikiwa na kuruhusu ujenzi kuanza mara moja.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma