Na. Mwandishi wetu, Kinshasa DRC Wakati Kanisa Katoliki nchini Tanzania likifanya ibada maalumu kumkumbuka Rais…
Na. Mseke Dide, Goma- DRC
Wafanya kazi watatu (3) wa Umoja wa Mataifa waufariki dunia mjini Butembo jumanne hii Kaskazini mwa mji wa Goma kupitia maandamano ya hasira yaliyoendelea katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Maandamano hayo yanayoendana na ghasia, uhalibifu wa mali na uporaji yanafanywa na raia hususani vijana wanaolituhumu jeshi la Umoja wa mataifa MUNOSCO kushindwa kudhibitii vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na vikundi vya waasi katika eneo la mashariki mwa DRC.
Tazama Video hapa
“Sisi Raia wa Congo tunaoishi mashariki mwa nchi tumechoshwa na hali ya ukosefu wa usalama haswa mauwaji yanayofanywa Na makundi ya kigaidi bila ya tume hilo la Monusco kuyazuia, sasa tumemeamua wenyewe kuwa majeshi haya yaondoke katika nchi yetu” alisisitiza mmoja wa waandamanaji .
Wameongeza kuwa MUNOSCO wameshindwa majukumu yao yakulisaidia jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo FARDC kuyatokomeza makundi yote ya uasi licha ya uwepo wao sehemu hiyo kwa zaidi ya myaka 20.