skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Watu 19 akiwemo marubani wawili waliofariki jana wakati wakisafiri na ndege ya shirika la ndege la Precision Air ya nchini Tanzania iliyopata ajali katika ziwa Victoria mkoani Kagera nchini Tanzania leo wameagwa rasmi katika mazishi ya kitaifa yakiongozwa na Waziri mkuu wa Tanzania Kassim majaliwa. Mwandishi wetu Prosper Kwigize ametuandalia taarifa ifuatayo

Ni majonzi na masikitiko kutokana na vifo vya watu 19 waliofariki jana katika ajali mbaya ya ndege iliyoanguka majini ndani ya ziwa vitoria umbali wa takribani mita 500 kabla ya uwanja wa ndege wa Bukoba kaskazini magharibi wa Tanzania

Akitoa taarifa kwa Waziri mkuu kuhusu tukio la ajali hiyo ya ndege, mkuu wa mkoa wa Kagera Bw. Albert Charamila ameeleza kuwa ndege hiyo ilikuwa na watu 43 ambapo 39 walikuwa abiria na 4 walikuwa ni watumishi na marubani wa ndege hiyo

Pamoja na mambo mengine Serikali imewapongeza wavuvi waliojitokeza kwa hiyari kuingia ziwani na kushiriki haraka kazi za uokozi na serikali imetoa zawadi kwa kijana aliyekuwa wakwanza kujitosa majini na kusaidia kuufungua mlango wa ndege na kuanza kuwatoa majeruhi, Mkuu wa mkoa anatumia nafasi hiyo kuiomba serikali kutenga bajeti ya mfuko wa maafa kuwapa mafunzo wavuvi hao juu ya namba ya kujiokoa na kuokoa wengine.

SIKILIZA RIPOTI KAMILI KATIKA SAUTI HAPA CHINI

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma