skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Wakati kukuwepo na sintofahamu ya upungufu wa mahitaji kwa wakimbizi kutoka Burundi na DRC wanaoishi mkoani Kigoma, hususani upungufu wa chakula, serikali imewaonya kutotumia mwanya huo kutoka nchi ya kambi zao kwa kisingizio cha kutafuta mahitaji ya ziada.

Onyo hilo limetolewa na Mratibu wa idara ya wakimbizi wa Kanda ya magharibi Bw. Nashon Makundi wakati akizungumza na BUha Fm na kusisitiza kuwa serikali ya Tanzania inatambua upungufu wa chakula katika kambi za wakimbizi na kwamba hali hiyo inatokana na kupungua kwa wahisani na mlipuko wa vurusi vya corona.

Bw. makundi amesisitiza kuwa, maisha katika kambi za wakimbizi yanatawaliwa na sheria za nchi na kwamba kwa mujibu wa sheria hizo mkimbizi haruhusiwi kutoka nje ya kambi kwa ajili ya kutafuta chakula wala kuni kwa kuwa huduma hizo hutolewa na umoja wa mataifa kupitia mashirika mbalimbali.

Amesisitiza kuwa mkimbizii anaweza kutoka nchi ya kambi kwa sababu maalumu ikiwemo matibabu katika hospitali ya rufaa na si kwenda kufanya shughuli za kijamii.

Wakimbizi kutoka Burundi na DRC katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma

Inaelezwa kuwa kutokana na changamoto ya upungufu wa chakula na nishati ya kupikia kwa wakimbizi katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli, kumekuwepo na msukumo wa wakimbizi kutoka ndani ya kambi kwenda katika mapori ya vijiji jirani kwa ajili ya kutafuta kuni na wengine kujitafutia ajira ndogondogo ili kupata fedha kwa ajili ya kununua chakula cha nyongeza, hata hivyo wakimbizi wanalalamikia uvunjifu wa amani kutokana na vizuizi vilivyowekwa kuwazuia wakimbizi kutotoka nje ya kambi.

Wakimbizi wengi wako njia panda wakisubiri amani ili warudi nyumbani, wengine wameshakata tamaa wangependa kupata hifadhi nchi ya tatu ambako fursa zinatajwa kuwa duni, lakini wapo wanaoona fahari kupata uraia wa Tanzania endapo watapewa fursa ya kufanya hivyo.

Hivi karibuni shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini tanzania lilikiri kuwepo kwa upungufu wa chakula na kubainisha kuwa juhudi mbalimbali zinafanyika ili kuwapunguzia wakimbizi adha na madhira yanayotokana na upungufu huo, huku mkuu wa UNHCR nchini Tanzania Bw. Antonioo Canhandula akitaja kuwa UVIKO 19 (COVID-19) NDIYO CHANZOO CHA KUPUNGUA KWA MISAADA YA WAKIMBIZI.

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wengi wangependa kurejea nchini mwao lakini hadi sasa wanashindwa kufanya maamuzi kutokana na hali ya usalama katika maeneo mengii ya mashariki kutokuwa tulivu.

Sango Msebengi ameiambia Buha kuwa yeye ni miongoni mwa waliochoka kuishi maisha ya ukimbizi kutokana na kukosa uhuru wa kujishughulisha au kutoka nje ya kambi

Sango Msebengi, Mkimbizi kutoka jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeishi kambi ya Nyarugusu

Nilikuja hapa kambini nikiwa kijana mdogo sana nikiwa na umri wa miaka 12 na sasa nimefikisha miaka 35 nikiishi ukimbizini, nazeekea humu kambini, majengo yote unayoona humu yamejengwa naona, natamani kurudi kwetu maana hapa sina uhuru hata wa kutoka nje ya kambi, nikitoka ni kipigo” Anasema Sango msebengi mama wa watatuu watatu.

Mkoa wa Kigoma una jumla ya kambi tatu za wakimbizi zenye idadi ya wakimbizi wapatao 230,000 kutoka nchi za Burundi na DRC na kwa sasa wakimbizi wengi wa Burundi wanajiandikisha kwa hiyari kurejea nchini mwao

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma