Na. Irene Bwire -PMO na Anita Balingilaki Buha - Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka…
Na. Matinde Nestory, Mwanza
Waumini wa dini ya kiislam mkoani Mwanza wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mwanza wameshiriki siku ya Eid Elftri kwa kutoa chakula kwa watoto yatima na watoto waishio mazingira magumu
Akifungua sherehe hiyo leo Mstahiki Meya Constantine Sima amesema kuwa dhamira ni kushiriki chakula Cha pamoja na watoto hao ili inasaidia kuonyesha upendo na mshikamano kwa watoto bila kujali dini zao
“Sisi Kama serikali tunatambua na tunawajibu wa kuhakikisha kwamba kundi hilo maalum tuendelea kulitunza na tunaamini kwamba yatima wa leo ni mzazi wa kesho“amesema Meya Sima.
Kwa upande wake Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke amesema kuwa hakuna mtaa unaozaa mtoto hivyo tuwatunze watoto tuwapende na kuwathamini watoto hii itasaidia kupunguza ongezeko la watoto wa mtaani.
“Jamii inatakiwa ikae na watoto yatima majumbani kwetu ni Jambo Bora zaidi lenye baraka zaidi kwa Mungu kuliko kuwalea kwenye vituo na kuwaacha wakizurura mtaani “amesema Sheikhe Kabeke.
Hata hivyo amewataka waislam kuendelea kuyaishi Yale yote waliyojifunza katika kipindi Cha mfungo mtukufu wa ramadhani kwa kutoa sadaka kwa wahitaji.
Nae Mkurugenzi wa Rock solution limited Zakaria Elias Nzuki amesema kuwa amekuwa akijitolea kuwasaidia watoto yatima na waishio mazingira magumu kwa Mkoa wa Mwanza na sehemu mbalimbali hii inasaidia kuongeza upendo dhidi ya watoto na anatoa wito kwa viongozi na wadau wengine kuwajali watoto na watu wanaoishi katika mzaingira magumu
“Katika siku Kama hii maalumu huwa tunajitolea kushiriki nao chakula cha pamoja na kufanya mambo mbalimbali ambayo tumekuwa tukifanya ni mwaka wa nne mpaka Sasa kila Mwaka mpya na siku ya Eid” amesema Nzuki.
Aidha amewaomba watu mbalimbali wajitokeze kuwasaidia watoto yatima na waishio mazingira Elimu na Mavazi hii itasaidia kupunguza wimbi la watoto waishio mtaani.
Mmoja wa watoto waishio mazingira magumu Joseph Isack Jeremiah kutokea Geita amesema kuwa changamoto ni nguo ambazo zimekuwa zikiwaishia,Mvua ikinyesha ,kukimbizwa na pa kulala, kufanyiwa ukatili hali ambayo inatishia afya zao.
Ameiomba jamii kuwasaidia mahitaji mbalimbali ikiwemo kuwapatia Elimu,Mavazi na Maradhi hii itasaidia kuondoa ongezeko la watoto waishio mtaani.