Na. Irene Bwire -PMO na Anita Balingilaki Buha - Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka…
Na Kibada Ernest -Mlele Katavi.
Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Association For the Development of Protected Areas (ADAP) Tanzania limeanza kusaidia Jumuiya ya wafuaga nyuki Inyonga kupitia vikundi vyake kusaidia kusindika uyoaga pori kwa njia ya kitalaam kwa kutumia Nishati ya Jua itakayokuwa ikitumia kifaa maalum kiitwacho Solar Draya
Shirika hilo limekuja na mpango huo baada ya kuona wafugaji wanaofugia mizinga yao porini hawanufaiki na zao la uyoga linaloharibika ambalo lingeweza kuwasaidia kwa chakula na kuwaingizia kipato kwa kuwa uyoga pori ni muhmu kwa afya na unaprotini za kutosha pamoja na vitamin katika mwili wa binadamu hasa kwa akinamama wajawazito.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa ADAP) Tanzania DKT, Vicent Vyamana, wakati akizungumza muda mfupi baada ya kutambulisha mradi wa uhifadhi Mazingira Utakaosaidia vikundi vya wafuga nyuki katika wilaya ya Mlele, Nsimbo na Sikonge kisha walitembelea eneo la ufugaji nyuki la Jumuiya ya wafugaji nyuki ya IBA linaljumuisha vikundi vya wafuga nyuki na kujionea shughuli inayofanyika katika eneo hilo.

Dkt Vyamana ameendelea kueleza watanunua majokofu matatu ya kuanzia kwa ajili ya wafugaji wa nyuki ambayo watayatumia kwa ajili ya kukaushia uyoga pori ambao ni Chakula watakuwa wanauvuna kutoka katika mashamba yao ya kufugia nyuki kisha kukausha na kuuhifadhi kwa ajili ya chakula na mwingine kuuza na kujipatia kipato.
Wakati wakijishughulisha na ukaushaji wa uyoga na utundikaji mizinga uhifadhi wa mazingira utakuwa ukiendelea kwa kuwa wanafundishwa kufunga nyuki na kuhifadhi mazingira katika maeneo wanayofugia nyuki.
Awali Mwenyeikiti wa Jumuiya ya wafuga nyuki kutoka kijiji cha Masigo Oscar Makolofila kwa niaba ya wafuga nyuki alieleza baadhi ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa mitaji ya kuendeshea shughuli zao za ufugaji,ucheleweshwaji kupatikana vibali vya kuingia porini maeneo wanakofugia nyuki wanapotundika mizinga yao, kwani wanapoomba, vibali kutoka kwenye Mamlaka za usimamzi wa Mistu hawapewa kwa wakati hali inayowafanya kutofanya kazi zao kwa wakati kwa kuwa ulinaji nao unaendana na msimu..

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka kutoka OR-TAMISEMI Idara ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali Dkt Masanja ameelekeza Halmashauri kuwasaidia wafugaji wa nyuki kwa kuwa mara nyingi miradi ya wafadhili huwa haiendelee pindi wanapoondoka na kuiacha miradi walioianzisha. Wafadhili wanawekeza fedha nyingi kwenye miradi lakini wanapoondoka mara miradi huwa haendelei.
Dkt Masanja ameeleza mfano hapa wafadhili wameweka fedha nyingi kwenye mradi huo wa ufugaji nyuki kupitia Jumuiya hii ya wafuga nyuki ya IBA ,na iwapo wakiondoka mradi huu unaweza usiendelee.
“Nashauri Halmashauri kuhakikisha wanawasapoti ili mradi huu uweze kuendelea kuwepo, na kuwanufaisha wananchi”alisema Dkt Masanja.
Pia amewashauri Wafuga Nyuki na kutumia fursa za Mikopo kutoka kwenye Halmadhauri inayotolewa kupitia Mapato ya ndani waombe mikopo hii kwa kufuata taratibu zilizowekwa watapatiwa ikiwemo kusajiri vikundi vyao mikopo ile haina riba serikali ya inayoongozwa na Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan inawajari wananchi wake zipo fedha za kutosha kuwakopesha kupita kwenye Halmashauri zitummieni.
Awali Katibu Tawala wilaya Wilaya Mlele Lincolin Tamba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe Filberto Sanga wakati wa kikao cha kutambulisha mradi wa uhifadhi mazingira amewataka wafadhili wanaotekeleza miradi kuweka uwazi ili kuondoa sitofahamu kwa jamii na jamii nayo itoe ushirikiano kwa kuwa miradi hiyo ni ya kwao.
Mwisho.