skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Bakingilaki,Maswa

Waziri wa mifugo na uvuvi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ng’ombe wengi lakini tija inayotokana na mifugo hiyo ni ndogo.

Amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Madeco mjini Maswa huku akiongeza kuwa Tanzania ni ya pili kwa Afrika lakini ikilinganishwa na wenye ng’ombe kidogo bado tija ni ndogo.

Kuhusu sekta ya uvuvi waziri Ndaki amesema Tanzania ina vyanzo vya maji vingi ambavyo vinaweza kufugia na kuvua samaki lakini bado tija ni ndogo pia.

Mheshimiwa Mashimba Ndaki Waziri wa Mifugo

“Ili sekta hizo mbili ziweze kuwa na tija kwenye taifa letu..sisi ni wenye ng’ombe wengi katika Afrika ni wa pili lakini tija ni ndogo ukilinganisha na wenye ng’ombe kidogo, tuna vyanzo vya maji vingi ambavyo tungeweza kufuga samaki na kuvua samaki lakini bado tija yetu ni ndogo, sasa mhe Rais ametuelekeza kwamba badilisheni ili sekta hizi mbili ( mifugo na uvuvi) ziweze kuchangia kwa sehemu kubwa kwenye pato la taifa na pato la wananchi” amesema waziri Ndaki.

Waziri Ndaki ameyataja mambo matatu ambayo watayafanya ambapo upande wa mifugo wameamua wafugaji watoka kwenye kuchunga/ kuswaga na badala yake waende kwenye kufuga.

“Kuna watu wanafikiri wanafuga kumbe wanachunga/wanaswaga ng’ombe na hawa ni wengi kwenye taifa letu…sasa tumeanza mfumo wa mabadiliko kwenye sekta ya mifugo tunataka kuwapeleka wafugaji wa nchi hii wawe wafugaji wenye tija kutoka kwenye ufugaji wao na hapa yatafanyika mambo matatu ambayo ni pamoja na kubadilisha aina ya mifugo tuliyonayo (mifugo tuliyonayo ni ile midogo yenye kilo kidogo) ukikamua unapata nusu lita au robo na kwa kuanza tumeanza na wilaya ya Maswa ambao tayari wamepokea madume ambayo yanaweza kubadilisha aina ya mifugo tuliyonayo”.

Mhesimiwa mashimba Ndaki (MB) na waziri wa Mifugo akiteata jambo na mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dr. yahaya Nawanda (kushoto)

Aidha wanatarajia kuwatumia wataalam kuhimirisha kwa njia ya chupa ili kuweza kubadilisha aina ya mifugo ikiwa ni sambamba na na kuleta majike ili mabadiliko ya aina yawepo kwenye mifugo iliyopo.

Mbali na hivyo waziri Ndaki amesema wanataka sekta ya mifugo iweze kutengeneza ajira nyingi kadri iwezekanavyo na kwa kuanza wameanzisha programu inayoitwa SAUTI PROGRAMU SAMIA UFUGAJI KWA TIJA na kupitia programu hiyo wanawachukua vijana wenye juhudi ya kufuga na kuwaweka kwenye vituo na kuwaelekeza sambamba na kuwanunulia ng’ombe.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa kwasasa baadhi ya wafugaji wanafuga kwa kuhamahama hivyo wanataka kubadilisha utaratibu na kwa kuanza watawamilikisha wafugaji ardhi na tayari wizara hiyo imekuja na mpango wa kuwaelekeza/ kuwafundisha namna ya kuotesha malisho kwenye maeneo yao na tayari yapo mashamba darasa zaidi 100 ambayo yameanzishwa kwenye baadhi wilaya ili yatumike kama vituo vya mafunzo kwa wafugaji huku akiongeza kuwa wanataka kubadilisha sekta hiyo ili iwe inatoa mchango mkubwa kwa taifa na uchumi wa mwananchi mmojammoja.

Viongozi wa Chama cha Mapinduci CCM waliohudhuria maadhimisho ya miaka 46 ya CCM na kupewa ujumbe mahususi kuhusu ufugaji kuwa wa kisasa na wenye tija, Mkoa wa simiyu unaundwa na makubdi makubwa ya wafugaji na wengi wao wanakabiriwa na tatizo la marisho

Kuhusu sekta ya uvuvi waziri Ndaki amesema wafugaji waachane kutumia njia moja ya kuvua samaki na badala yake waanze kufuga kwa kutumia vizimba na mwaka huu tayari wamepokea kiasi cha shilingi bilioni 11 kutoka serikalini kwaajili ya vizimba na hapo ajira zitapatikana na tayari kuna wanufaika zaidi 1800.

Mbali na hilo wanaenda kupandisha hadhi mabwawa yaliyopo nchini na miongoni ni mwa mabwawa hayo lipo la Zanzui wilayani Maswa ambapo watapanda samaki kila eneo lenye maji ili wananchi wapate lishe na maji.

Aidha wameanzisha vituo vya ufugaji wa samaki kwenye wilaya 100 nchini na vituo hivyo watakuwepo wanaojifunza wakihitimu wanaenda kufuga samaki wao.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma