skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na kupongeza kwa kuwepo na mageuzi katika tasnia ya habari barani Afrika, amewaonya waandishi wa habari wa kiafrika kuacha kutumiwa na vyomboo vya habarii vya magharibi kuzichafua nchi zao wenyewe wakati wanaowahimiza kufanya hivyo wakizuia mambo yao yasijulikane.

Rais Samia amesema hayoo leo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari ambayo katika bara la Afrika yamefanyika Mjini Arudha nchini Tanzania, yeye akiwa mgeni rasmi.

Rais Samia amebainisha kuwa wanahabari wa kiafrika wamekuwa sehemu ya kulichafua bara la Afrika badala ya kuandika masuala yanayochochea maendeleo, wengi wao huandika na kulichafua bara hilo mbele ya uso wa wageni.

“Ninyi mnatumiwa na mataifa ya kigeni kuwapa taarifa za hovyo kuhusu bara letu, mnajivua nguo wenyewe wakati mnaowapa hizoo taarifa waoo za kwao wanahakikisha hamzijui, wanaficha lakini zenu zinazohusu maslahi ya mataifa yenu mnawapa, huku ni kujivua nguo mwenyewe, mbona wao hawawapi za kwao? hata kama mnapewa fesha au vitu au mnatafuta sifa jiulizeni,, je! wao wanafanya hivyo kwa kuwapa taarifa za nchi zao? alisisitiza Rais Samia katika hotuba yake

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia umma wa waandishi wa habari kutoka barani Afrika wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo cya habari duniani mjini Arusha

Amesisitiza kuwa bara la afrika sawa la yalivyo mabara mengine yana mambo yake na zipo fursa na utajiri mwingi wa mali asili ikiwemo misitu na mbuga za wanyama ambavyo havipewi kipaumbele na vyombo vya habari vya magharibi na vyombo vya afrika navyo havifanyai jitihada kutangaza utajiri wa afrika badala yake wengi huandika habari zisizoleta matokeoo chanya.

Kuhusu changamoto za sheria nchini Tanzania, Rais Samia ameelekeza wizara ya habari kushirikiana na wadau wa habari kuhakikisha Sheria za Habari ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kubinya uhuru vya vyombo vya habari znairekebishwa.

“Nimeelekeza Sheria zirekebishwe lakini kwa majadiliano pande zote na si tu kwamba sisi tunataka nini. Nimemwelekeza Waziri (Nape Nnauye) sheria za habari zirekebishwe kwa kushirikisha wadau wote ili kila upande utoe mchango wake juu ya kipii kirekebishwe kwa kuzingaia maslahi ya pande zote”,amesema Rais Samia.


Rais Samia akimnukuu waziri wa habari amesisitiza kuwa Tanzania na hata mataifa mengiine ya Afrika zinatumia busara  lakini sheria zipo pale pale.

Busara ninayotumia, ukinikuna vizuri mimi nitakupapasa huku nakupuliza, lakini ukipara nitakuparura, tufanye kazi kwa uungwana, na kwa kuelewana”, Waandishi wa habari mna mchango mkubwa katika maendeleo, kwanini mimi nifanye kazi bila waandishi wa habari. Hivyo hatuhitaji kugombana, tukae tuzungumze tujenge nchi yetu, Kuna sheria zinawalinda lakini jilindeni wenyewe“,amesema Rais Samia.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samiaa Suluhu Hassan amefanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari kwa kipindi kifupi cha mwaka mmmooja tangu alipngia madarakani na kwamba seikali ina nia ya dhati ya kuweka mazingira mazuri ya waandishi wa habari na vyombo vya habari

hata hivyoo ametahadharisha kuwa Sheria na Kanuni zilizotungwa na kupitishwa hata kama zina mapunufu hazijafutwa na kwamba busara inatumika katika kusimamia tasnia ya habari.

Tunatumia busara ili mambo yaende. Busara hii ni vizuri ikaheshimiwa. Msinitie majaribuni, naomba mnisaidie tupite kwenye kipindi cha mpito salama wakati tukipitia maboresho ya sheria hizi, tutahakikisha maoni ya kila mtu yanalindwa”,amesema Waziri Nnauye.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma