skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Vijana kadhaa kutoka mkoani Kigoma wamepongeza shirika la maendeleo la OHIDE Tanzania kwa kuamua kuanzisha mradi wa mawasiliano kwa njia ya Radio na kuomba mamlaka husika kuunga mkono juhudii hizo kwa ajili ya maendeleo ya mkoa wa Kigoma

Promise Wagwene

Vijana hao wapatao kumi wametoa pongeza hizoo baada ya kutembelea studio za kituo cha Radio cha BUHA kinachotarajia kuanza kurusha matangazo yake hivi karibuni kutoka mjini Kasulu mkoani Kigoma.

Miongoni mwa vijana haoo ni waliopata ufadhili wa miradi ya ujasiriamali kutoka Umoja wa mataifa kupitia katika mpango wa pamoja na Kigoma maarufu kama Kigoma joint Program (KJP) ambapo miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania milioni mia saba ilifadhiliwa kwa vikundii vya vijana na wanawake katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko ambako wanahifadhiwa wakimbizi zaidi ya 250,000.

Wameeleza kuwa, endapo Radio hiyoo itaanza, miradii inayoendeshwa na vikundii vya wanawake na vijana itatangazwa na hivyoo kupata soko sambamba na kuwahamasisha wengine kuanzisha vikundii vya ujasiriamali tofauti na sasa ambapoo kutokana na kutokuwepo na kituo cha Radio shughuli za uhamasishaji na uelimishaji zinafanyika katika mazingira magumu na kwa gharama kubwa.

“Bidhaa zetu zinakosa soko kutokana na kutotangazwa, hivyo tunaamini kuwa kuanzishwa kwa BUHA FM ndio ukombozi wa Kigoma kwani upashanaji wa habari ni moja ya nyezo mhimu za kibiashara.

Vijana waliotembelea BUHA FM studio ni kutoka kikundi cha utengenezaji wa Mvinyoo wa ndizi maarufu banana cha MUSUASO kinachoundwa na wasomi kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA) na vijana wa kikundi cha utengenezaji wa viatu vya ngozii cha KAYORE pamoja na wengine kutoka Umoja wa vijana wa CCM wilaya ni Kasulu.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma