Na. Mwandishi wetu, Kinshasa DRC Wakati Kanisa Katoliki nchini Tanzania likifanya ibada maalumu kumkumbuka Rais…
Imeandikwa Na M’MOLELWA MSEKE DIDE -Buha FM, Beni, DRC
Jumatatu hii ya tarehe July 25 hali ilikuwa ya wasiwasi pamoja Na shughuli nyingi kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo hususan maeneo mengi ya mkoa wa Kivu ya kaskazini kufuatia mamia ya vijana kuandamana wakiyakosoa majeshii ya umoja wa mataifa yanayolinda amani nchini humo
Kisa na mkasa kwa vijana hao kuingia barabarani na kuvamia makazi ya askari hao ni mwito uliyo tolewa na makundi ya vuguvugu nchini humo kama vile mashirika ya kiraia yanayopinga uwepo wa vikosi kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa (Monusco) nchini humo kwa kile walicho kiita kuwa ni kushindwa kudumisha Amani tangu uwepo wao nchini DRC ikiwa sasa miongo miwili bila ya raia kufaidika na uwepo wa Umoja wa mataifa nchni humo

Waandamanaji hao wanadai kuwa licha ya kuwepo na askari wa kulinda amani, yameendelea kutokea matukio mengi ya uvunjifu wa amani na vitisho vya kiusalama ikiwemo mauwaji ya watu, utekwaji nyara, kuharibiwa kwa Mali na matukio mengine ya uhalifu dhidi ya binadamu
Vijana hao wenye hasira wamelalamikia zaidi kitendo cha waasi wa makundii mbalimbali kuachwa waivuruge Congo huku wakitaja waasi wa kundi la Allied Democratic Forces(ADF) kutoka Uganda, M23, FDLR Na wengine kuendesha uhalifu bila kuguswa na Umoja wa mataifa.
Kutwa nzima Barabara zilifungwa sehemu kadhaa kwa kuwekwa vizuizi hapa na pale kwenye baadhi ya barabara Kuu, kufuatia vijana kuchoma matairi ya magari na mapambano ya ana kwa ana na askari wa serikali ya DRC waliofyatua mabomu ya kutoa machozi ili kuwadhibiti waandamanaji hao ambao walikusudia kuvamia makao ya vikosii vya Umoja wa Mataifa mjini Goma.
Watu kadhaa wamejeruhiwa na wengine wamekimbilia kusikojulikana huku ikibainishwa kuwa moja ya majengo la MUNOSCO limechomwa motoo na waandamanaji wakishinikiza Umoja wa mataifa kuwaondoa wawakilishi wake Mashariki mwa DRC
Hasira za wenyeji zimechuwa kasi tangu msemaji wa tume la kulinda Amani nchi Drc (Monusco alipotangaza kuwa hawapo tayari kushambulia waasi wa M23 wanao shikilia Eneo muhimu la BUNAGANA kwenye mpaka wa Congo/Kinshasa Na Uganda kwa kuwa waasi hao wana vifaa vya kivita vya hali ya juu

Pamoja Na hayo, Mwenyekiti wa Baraza seneti nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Mh Bahati Lukwebo alipokuwa ziarani mashariki mwa nchi hiyo alikumbusha kauli ya msemaji wa Monusco Na kutangaza hadharani kuwa Tume hiyo imeshindwa kulisaidia jeshi la Taifa
Gavana Askari wa mkoa wa Kivu ya Kaskazini luteni Jenerali NDIMA KONGBA Costant akiwali jijini Beni kutoka Goma maskani ya mkoa huo, ameomba kuwaomba raia kuwa Na UTULIVU wakifajalu kuwa Monusco ilialikwa Na serkali yao,