skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Vijana wa Jiji la Mwanza wameungana na Bunge la Jamhurii ya muungano wa tanzania kutoa pongezi kwa rais wa jamhuri ya Muungano wa tanzania kwa kupata tuzo ya uongozi bora katika kusimamia ujenzi wa miundombinu kwa mwaka 2022 sambamba na kutoa zaidi ya shilingi Bilipni 1.7 za mikopo ya vijana wanawake na watu wenye ulemavu zimetolewa  na Serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha mwaka 2021- 2022 katika jiji la Mwanza.

Hayo yamebainishwa leo na mwenyekiti wa UVVCM wilaya ya Nyamagana Boniphace Zephania katika hafla ya kumpongeza Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kutokana na juhudii zake za kuliletea taifa maendeleo na kuwajali wajasiriamali

Bw. Zephani amebainisha kuwa pesa hizo za Mikopo  ni kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuletea maendeleo ya Taifa.

Baadhi ya vijana walioshiriki mkutano wa kutoa tamko la pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan jijini Mwanza mapema leo

Sambamba na hayo Boniphace amempongeza Rais Samia kuwa Rais wa kwanza mwanamke kupokea tuzo  nchini Ghana ambapo tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi wakuu wa nchi wanaofanya vizuri katika sekta ya miundo mbinu.

“tuzo aliyopewa rais wetu sisi kwetu tunaamini kupitia tuzo hii ambayo amepewa Rais Samia ni Tunu  kwetu  watanzania tuna uwezo wa kujivunia tuzo hiyo”Amesema Boniphace.

Boniphace amempongeza Rais Samia kwa kuimarisha Kikokoteo cha wazee kwa kufikia 33%, na kuendelea kujenga vituo vya afya, kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wadogowadogo (MACHINGA) na ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya usafiri na usafirishaji.

Aidha ameeleza kuwa Rais Samia ametoa milioni 500 kwa kila halmashauri nchini ili kuwawezesha wamachinga kukaa katika mazingira salama, huku akitoa bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za wamachinga kote nchini na kuimarisha miundombinu ya nchi kama Ilani CCM inavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kujali maslahi ya watumishi.

“Sisi Kama Jimbo la Nyamagana tunampongeza Rais Samia kwa kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi nchini kwa ongezeko la mshahara 23%” amesema Boniphace.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa chama cha walimu (CWT) wilaya ya Nyamagana  Mwl. Sholi Daniel Maduhu ameishukuru serikali na Rais Samia kwa kutoa ajira 32,000 kati ya ajira 45,000 kote nchini, kuboresha maslahi ya watumishi pamoja na kupanua wigo wa ajira.

“Sisi Kama chama Cha walimu wilaya ya Nyamagana tunampongeza Rais Samia kwa kuongeza Mishahara kwa watumishi wa imma hata Sasa tunauwezo wa kwenda sokoni tukiwa na furaha” amesema Mwl Maduhu.

Nae mwenyekiti wa Senet  ya vyuo vikuu Mwanza  Christian Kimaro amesema kuwa wanafunzi wamenufaika na bilioni 1.6 ya mikopo, maboresho ya vyuo  mbalimbali  hapa nchini pamoja na kutoa chanjo ya Uviko 19 ambayo imewasaidia baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa kwenda kusoma nje ya nchi.

Imeandaliwa na Matinde Nestory- Mwanza

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma