skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Ikiwa zimesalia siku Saba kufikia tarehe ya mwisho ya kusalimisha silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria Makamanda wa Polisi katika mikoa mbalimbali wanaendelea kuhamasisha wananchi kusalimisha silaha kabla ya muda huo.

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa ambavyo wananchi wake wanatakiwa kusalimisha silaha kabla ya Novemba 30. 2021.

Katika Mkoa wa Pwani leo Novemba 23, 2021 Kamanda wa Polisi ACP Wankyo  Nyigesa amesema muitikio wa wananchi wa kusalimisha Silaha unaendelea vizuri.

Hadi sasa Mkoa wa Pwani umepokea silaha za aina mbalimbali ishirini na nne na idadi inatarajiwa kuongezeka katika kipindi cha siku Saba zilizosalia.

“Katika Mkoa wetu Zoezi linakwenda vizuri na hii ni ishara njema ya ushirikiano na wananchi, mpaka Sasa kupitia maeneo mbalimbali tuliyoelekeza ambayo ni vituo vya Polisi na ofisi mbalimbali za kata, zimesalimishwa Rifle 2 na risasi 40, bastola 1 na risasi 7 pamoja na magobore 21,” amesema ACP Wankyo. Sikiliza sauti yake hapa chini


Wankyo amesema, zoezi la usalimishaji wa silaha limetekelezeka Kwa muda wa mwezi mkoja hivyo kwa wananchi ambao bado hawajasalimisha silaha wanazomiliki Kinyume na sheria wazisalimishe ndani ya muda uliotolewa baada ya hapo msako mkali utafanya na yeyote atakaye kamatwa atakuwa amekiuka sheria.

Ameongeza kuwa namna wananchi walivyojitokeza kuitikia wito katika mkoa huo, inatokana na jitihada kubwa zinazofanywa nanjeshi la Polisi katika kuweka ushirikiano na wananchi.

Katika hatua ingine jeshi la Polisi limekamata wanawake watatu kati ya  watuhumiwa 21 wanaume wakiwa 18 katika msako na doria uliyoanza Novemba 15 hadi Novemba 22 mwaka huu, wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ya wizi.

Pia Wankyo, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani kujitokeza na kubaini Mali zao zilizoibiwa wakiwa na vithibitisho, pamoja na kushirikiana na jeshi la Polisi katika kutoa ushahidi kwenye kesi hizo.

Kamanda huyo ametoa Rai Kwa watu mbalimbali kujituma katika kufanya kazi halali, badala ya kufanya matukio ya kihalifu, kwani yeyote atakayebainika atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria, maana Uhalifu haulipi.

Mnamo Octoba 30, 2021 waziri wa Mambo ya ndani ya nchi George SimbaChawene aliwataka wananchi wanaomiliki silaha Kinyume cha sheria kuzisalimisha silaha zao kuanzia Novemba 1 hadi Novemba 30. 2021.

Imeandaliwa na Mussa Mkilanya – Buha FM Pwani

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma