skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Joel Daud, Muleba

Wafugaji wilayani Muleba mkoani Kagera wameiomba Serikali kupitia wizara ya mifugo hapa nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mifugo kupeleka dawa na chanjo kwa mifugo baada ya mifugo wao kuugua ugonjwa unaotoboa midomo na miguu maarufu kama “Suuna” na kusababisha baadhi ya mifugo kufa

Rai hiyo imetolewa na Bw. Jeremia Wambura kwa niaba ya wafugaji wakati wa kikao cha wafugaji kwa wilaya ya Muleba kilichofanyika wilayani humo na kueleza kuwa kwa kipindi kirefu  ugonjwa huo  umekuwa ni changamoto na tishio kubwa  kwa mifugo wao hali inayopelekea kudhohofika ki afya na baadaye kufariki.

“Wafugaji wilaya ya Muleba tunashida ya ugonjwa huu wa kutoboa midomo na miguu suuna kwa mifugo wakiwemo Ng’ombe kwa mkoa wa Kagera unatuathiri sana wafugaji na huo ugonjwa una miaka mingi kwa mkoa huu na wilaya ya Muleba lakini dawa zake hazipo. Mpaka sasa kuna baadhi ya maeneo kwa wafugaji Ng’ombe hawali na hawanywi wamekonda na wengine wamekufa” Alisema Bw. Jeremia Wambura

Katika kuhakikisha ufugaji unakuwa mkombozi kwa kuwainua wafugaji walio wengi kwenye nyanja za kiuchumi katika wilaya ya Muleba mkoani Kagera, wafugaji hao waliiomba serikali kupitia kikao hicho kutatua tatizo hilo kwa kuwapelekea chanjo ikiwemo madawa ya kuongeshea mifugo wao ili kukabiliana na ugonjwa huo hatari kwa mifugo wao.

Kufuatia maombi ya wafugaji hao, afisa mifugo wilaya ya muleba Bw. Oscar Bitariho alisema kuwa chanjo ya ugonjwa wa miguu na midomo haiko kwenye orodha ya chanjo ambayo inazalishwa hapa nchini badala yake wameendelea kuwasaidia wafugaji kukabiliana na tatizo hilo

“Lakini chanjo ya ugonjwa wa miguu na midomo kwa wafugaji ni gharama kubwa kidogo kwa kweli tunawahudumia wale wanaokuja kwa hiari yao na kabla hawajaugua, tunafanya hivyo kwa kuwasaidia. Suala la dawa ya kuogesha yale maeneo yote ambayo yana majosho wameishachukua dawa ya kuogesha kwa hiyo suala la kuogesha siyo shida kwa Halmashauri ya wilaya ya Muleba”.Alisema Bitariho

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma