skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki, Simiyu

Wakulima mkoani Simiyu wamesema uwepo wa kituo cha umahiri cha usambazaji teknologia za kisasa za kilimo kilichopo  eneo la Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu kumewawezesha kuzalisha kwa tija tofauti na awali.

Wamesema uwepo wa kituo hicho kumewanufaisha kwa kupata elimu kutoka kwa wataalamu ambao wanapatikana kwa wakati ikiwa ni pamoja na kujifunza teknolijia mbalimbali ambazo wanazitumia kwenye mashamba yao na hivyo kuongeza tija kupitia uzalishaji wao.

Kuwepo kwa kituo hiki kumetunufaisha,tumepata elimu hapa tumejifunza mambo mbalimbali, mara nyingi tulikuwa tunalima kwa mazoea lakini kwasasa baada ya kupata elimu, hapa  ukifika unapata elimu ya kutosha, tumeanza kuzalisha kwa tija tofauti na awali tulikuwa tukilima kwa mazoea“Elia  Shingalo mkulima

Wameyasema hao mbele ya mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda na wataalamu kutoka Taasisi  ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), ikiwa ni siku ya mkulima shambani kwenye kituo cha umahili cha usambazaji teknologia za kisasa za kilimo kilichopo  eneo la Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani Simiyu.  

“Tunapokea wadau tofauti na wa rika tofauti ambao wanafika kujifunza wapo vijana wao zaidi wanafika kujifunza mazao ya bustani, watu wazima wengi ujifunza mazao ya chakula na biashara, mwitikio unazidi kuongezeka mfano kuna vikundi vinaungana na kuja kujifunza mazao tofauti wapo wanaokuja kujifunza kilimo cha mtama na wananunua mtama na kulima mmoja mmoja,tunatoa wito kwa wakulima wengine wafike  kituoni kwetu tunafanya kazi mwaka mzima hapa watapata elimu ya kutosha na kununua mbegu kwaajili ya kwenda kuongeza uchumi wao, na kupata chakula “Mrema

Naye mtafiti kutoka TARI  Ukiriguru Theodoro Thadei  amesema kituoni hapo pia wanaofika wanajifunza kilimo cha pamba ambalo ni zao la kimkakati nchini na wao (TARI) wanapofanya utafiti wanazingatia matakwa ya kila mdau huku akiwataja  wadau hao kuwa ni mkulima,kiwanda cha kuchakata pamba na kiwanda cha kusokota nyuzi na kutengeneza nguo za pamba.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda akipokea mbegu za viazi lishe kutoka wa msimamizi wa kituo cha Nyakabindi Isabela Mrema kwa ajili ya kuwagawia wakulima waliofika kituoni hapo

Kwa upande wake  Mratibu wa uhaulishaji wa teknologia kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Ukiriguru  Dkt. George Sonda  amesema Nyakabindi  ni kituo mahiri cha usambazaji wa teknolijia ambazo wamezifanyia utafiti ili ziweze kuwafikia walengwa (wakulima), na hapo wanateknolojia zinazojibu changamoto nyingi ambazo  wakulima wanakutana nazo ikiwa ni sambamba na sekta ya kilimo kwa ujumla kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Isabela mrema ni msimamizi wa kituo cha usambazaji wa teknolijia Nyakabindi amesema kituo hicho kimeanzishwa  mwaka 2021 na kinapokea wadau tofauti ambao wanafika kujifunza mazao tofauti kulingana na mahitaji yao huku akiongeza kuwa mwitikio wa wananchi kutoka kwenye  mikoa mitatu ya kanda ya ziwa Mashariki ambayo ni Simiyu,Shinyanga na Mara ni mkubwa na mpaka Marchi 3,2023 wametembelewa na  wakulima 3121 wakiwemo wanawake 750 na wanaume 2371 kutoka mikoa hiyo inayohudumiwa na kituo hicho.

“ Tunafahamu mabadiliko ya tabia nchi yanakuja na madhara yake mbalimbali ikiwemo magonjwa,ukame ,siku hii ya mkulima tumetoa elimu kwa wakulima wote waliofika kutoka halmashauri zote za mkoa wa Simiyu, wamejionea teknolojia mbalimbali ambazo tunazitoa hapa kwa vitendo tunayo mashamba darasa, tunawasisitiza wakulima waendelee kutumia teknolojia ambazo tunawashauri na kawahamasisha ili kuondokana na changamoto, tunazo mbegu zinazostahimli ukame yakiwemo mahindi tunazo mbegu za mazao mbalimbali zinazokomaa mapema na zenye tija ”amesema Dkt Sonda.

Kuhusu namna teknolojia zinavyowafikia wakulima Dkt Sonda amesema wanashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo  halmashauri zote mkoani hapo  na hadi sasa zimewafikia wadau 3121 na hao wamefikiwa moja kwa moja .  

Mkuu mkoa wa Simiyu Dkt  Yahaya Nawanda amewataka wakulima na wananchi mkoani humo kuendelea kukitumia kituo hicho na wataalam waliopo ili wapate maarifa yatakayowasaidia kuongeza uzalishaji na kuondokana na umasikini huku akiongeza ni kituo cha TARI Nyakabindi kinazalisha teknologia nyingi za kisasa za kilimo ikiwemo mbegu bora ambazo zinamanufaa kwa wakulima.

“Nichukue hii nafasi kuwaombeni wananchi tuendelee kutumia hiki kituo lakini wataalam hawa tuendelee kuwatumia kwani wana maarifa mazuri lengo letu tuongeze uzalishaji tukishaongeza uzalishaji tutaondokana na umasikini, fikeni kwa wingi kwa ajili ya kujifunza mtapata mbegu bora za kisasa, mtazalisha kwa tija” amesema Dkt Nawanda

Katika hatua nyingine Dkt Nawanda  akawataka wakulima kutouza chakula chote kitakachopatikana kwani hali ya hewa ya msimu huu sio nzuri, kutokana na hali hiyo, wakulima hawana budi kuacha kuanza kuuza chakula, na badala yake wakitunze ili kuweza kukitumia wao pamoja na familia zao kwani uzalishaji utakuwa kidogo.

“Mwaka huu mvua zenyewe mnaziona zilivyo sio nzuri sana kwahiyo hata hiki chakula kichache ambacho tutafaidika kupata basi naomba wananchi wangu kwa uwezo wa MUNGU tusiuze chote.” ameongeza Dkt  Nawanda.

Katika hatua nyingine wakulima wote waliofika kituoni hapo wameweza kupatiwa mbegu za viazi lishe kwaajili ya kwenda kupanda kwenye maeneo yao.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma