skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Tanzania imetajwa na kupongezwa kwa kufanya mageuzi katika kutoa fursa kwa vyombo vya habari kufanya kazi zake kwa uhuru ingawa inaelezwa kuwepo kwa changamoto kadhaa

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania Bw. Deodatus Balile wakati wa uzinduzi wa kongamano la siku ya Uhuru wa habari duniani ambayo katika bara la Afrika maadhimisho hayo yanafanyika katika jiji la Arusha nchini Tanzania

Balile amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita tanzania imeyarushusu magazeti matatu (3) yaliyokuwa yamefungiwa kuendelea kutoa huduma huku vizurizi vya kanuni na sheria za uchapishaji mitandaoni nazo zikifanyiwa mageuzi

Tunafurahi sana kuona kuna mageuzi kadhaa ya mazingira ya kufanya kazi za habari nchini Tanzania, na niwahakikishie wadau na wageni kutoka katika mataifa mbalimbali barani Afrika kwamba tanzania sasa ni Salama kwa wanahabari kuliko ilivyokuwa mwaka mmooja uliopita, nawaondoa hofu na kuwatakiwa furaha ndani ya Tanzania.

Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya habari na msemaji mkuu wa serikali Bw. Gerson Msigwa ametoa pongezi kwa waandaaji wa kongamano hilo na kuweka bayana kuwa serikali ya Tanzania inaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wanahabari na vyombo vya habari kufanya kazi kwa uhuru.

Msigwa amebainisha kuwa, milango ya majadilinao panapotokea changamoto iko wazi wadau kujadiliana na serikali namna bora ya vyombo vya habari kufanya kazi kwa uhuru na kwa weledi zaidi kwa manufaa ya pande zote mbili.

Tasnia ya habari ni moja ya taaluma mhimu sana Tanzania na kama ilivyo katika nchi nyingine duniani, inatakiwa iheshimike na uandishi wa habari ufanywe na watu wenye taaluma hiyo ili kuipa heshima tasnia hii. Mimi niinaiheshimu sana na ni mwandishi wa habari na pamoja na majukumu yangu naendelea kuipenda taaluma ya habari. Alisema Msigwa msemaji mkuu wa Serikali

Zaidi ya wanahabari 1000, viongozi wa vyombo vya habari na wadau wengine barani afrika wanahudhuria kongamano hilo linaloratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo MISA, TEF, MCT na UTPC.

Kilele cha maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani ni Mei 3, na Rais Samia Suluhu Hassan wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Mjadala mkuu katika maadhimisho ya mwaka huu ni kuhusu Uandishi wa habari na changamoto za Kidijiti (Digital).

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma