WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua jengo la wagonjwa wa dharura kwenye hospitali ya wilaya ya…
Huduma ya Radio barani Afrika zimepongezwa kwa namna zinavyotoa huduma za utangazaji na kuzisaidia serikali kuwafikia wananchi sambamba na kudumisha Amani
Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa Habari, mawasiliano nanteknolojia ya habari nchini Tanzania Bw. Kundo Mathew wakati akifungua kongamano la utangazaji la mwaka 2023 jijini Dodoma
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule amekiri kuwa urahisi wa serikali kuifikia jamii ktk masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumu, kiusalama na kisiasa kumekuwa rahisi kutokana na namna waandishi wa habari wa Radio wanavyowasilisha maudhui sambamba na kuaminiwa kwao na urahisi wa jamii kusikiliza radio ukilinganisha na vyombo vingine
Wamiliki na viongozi wa radio nchini Twnzania wao wana maoni gani kuhusu huduma za radio na mchango wake kwa maendeleo? Dr. Godfrey Akigawesa ni mkurugenzi wa Karagwe FM kutoka mkoani Kagera mpakani mwa Uganda na Rwanda ambako Radio ikiwahi kutumika vibaya na kusababisha machafuko nchini Rwanda, yeye anakiri kuwa radio zina mchango mkubwa katika kukuza ustawi wa jamii na usuuhishi
Je! Ni kwa namna gani Radio inachangia kudumisha na kushawishi uwepo wa amani katika mataifa yenye migogoro? Je ! Ipo fursa kwa mataifa yenye migogoro kutumia Radio na kurejesha Amani. Brother Edwin Mpokasye ni kiongozi wa Radio Fadhila inayomilikiwa na shirika la Franciscan la kanisa Katoliki nchini Tanzania
Mwandishi wetu Prosper Kwigize ametuandalia ripoti kuhusu siku ya radio duniani kutoka Dodoma Tanzania. Bofya kwenye picha ili kusikiliza
Siku ya Radio duniani huadhimishwa kila mwaka Feb 13 kama sehemu ya azimio la umoja wa mataifa na siku hii inaratibiwa na shirika la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO