skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Wadau wa maendeleo, Jeshi la Polisi na makundi ya watoto wanaopinga ukatili mkoani mwanza wameitaka jamiii kutojihusisha na vitendo ya ukatili dhidi ya watoto ambavyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu .

Rai hiyo imetolewa June 16 mwaka huu katika Maadhimisho ya Siku ya mtoto wa Africa yanayofanyika kila ifikapo June 16 katika uwanja wa furahisha jijini Mwanza yenye kauli mbiu Tuimarishe Ulinzi wa Mtoto Tokomeza  Ukatili Dhidi yake,Jiandae Kuhesabiwa.

Mmoja  wa wadau ambaye ni mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Beyond  Giving  Tanzania Bw. Joseph Msuka ambao wanajihusisha na watu wenye ulemavu alisema kuwa jamii inapaswa itambue kuwa mtoto mwenye ulemavu ni sawa na mtoto mwingine hasa kwenye Elimu na Afya ( Matibabu)

Bw. Joseph Msuka mkurugenzi wa shirika la Beyond Giving Tanzania linalohudumia watoto wenye ulemavu Jijini Mwanza

Bw. Msuka alibainisha kuwa watoto wenye ulemavu wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya kikatili ambayo vinaanzia ndani ya familia kwenda kwa jamii huku wakiamiinishwa kuwa kuwa na mtoto mwenye ulemavu ni mkosi au laana ambavyo vinatishia maisha ya watoto hasa walemavu.

Ameongeza kuwa kupitia shirika hilo ambalo linahudumia watoto 67 kutoka wilaya za Magu, Ilemela pamoja na Nyamagana ambapo wanatoa Elimu ya  mafunzo kwa watoto wenye ulemavu kwa wazazi au walezi, kuwakatia bima za afya ya shilingi 50,400 pamoja na jamii itambue haki zao za msingi za watoto wenye ulemavu.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la Action For Community Development (ACODE) Winner Chimba amesema kuwa kupitia shirika hilo ambalo linajihusisha na tiba tengemao kwa watoto wenye ulemavu pamoja na kuwapa ujuzi kazi kwa vijana wenye ulemavu hususani wenye matatizo ya akili.

Ameongeza kuwa wazazi wanatakiwa kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu kwa kutowapa Elimu na kuwaona ni mkosi katika familia hali ambayo inatishia maisha ya watoto hao.

Wakati huo huo  Mkurugenzi wa Taasisi  ya Living Together Autistic Foundation Mhandisi Shangwe Mgaya amesema kuwa kupitia shirika hilo ambalo linajihusisha na watoto wenye usonji amesema kuwa wametoa bima za afya 70 kwa watoto wenye changamoto hiyo ambapo watoto hao wanahudumiwa  tiba ya viungo,tiba ya kuzungumza, bingwa wa mfumo wa fahamu pamoja na tiba ya tabia.

Mhandisi Shangwe Mgaya Mkurugenzi wa shirila la Living together Autistic Foundation

” Tuimarishe Ulinzi kwa watoto wenye changamoto ya usoji wamekuwa wakifanyiwa ukatili mbalimbali ikiwemo kuchomwa Moto,kuvunjwa miguu kutokana na zile tabia wameona ni mzigo pamoja na  jamii itambue kuwa mtoto mwenye usonji akifundishwa anafundishika”amesema Mhandisi Mgaya.

Nae Mwanasheria wa shirika la Railway Children Africa (R.C.A)  Judith Kasera amesema kuwa shirika hilo ambalo linajihusisha na watoto wanaoishi katika mazingira ya mtaani wanasimamia misingi na usalama wa mtoto kwa kusimamia Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 Kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

“Sisi Kama shirika tunafanya nao kazi moja kwa moja mtaani na kuhakikisha tunafatilia Ulinzi na usalama wao kwa wale walio tayari kurudi majumbani, ambapo familia ndio sehemu salama kwa ajili ya Ulinzi wa mtoto”amesema Kasera.

Sanjari na hayo imeitaka jamii kutowaficha watoto wenye ulemavu sababu Sheria ya nchi inatambua usawa wa watoto wote na wanahitaji Ulinzi Kama watoto wengine.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma