skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Habari na Ananias Khalula.

Waandishi wa habari saba (7) kutoka mikoa mbali mbali chini Tanzania wanashiriki mafunzo ya uandishi wa habari unaozingatia maslahi ya Jamii na kuleta matokeo chanya kwa umma

Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza oktoba 24 mwaka huu katika ukumbi wa kituo cha  Buha Radio FM yanahusisha wanahabari  kutoka mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Dar es salaam kwa hisani ya shirika la maendeleo na uewekezaji OHIDE

Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiwa darasani

Bw. Prosper kwigize ambaye ni mwezeshaji katika mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo  yanalenga kuwaandaa waandishi wa habari vijana kujua namna ya kuandika habari ambazo zinagusa na kuleta matokeo kwa wananchi.

Katika hatua nyingine ameeleza  kuwa kuanzishwa kwa kituo cha buha radio fm katika wilaya Kasulu mkoani Kigoma kutasaidia wanchi wa kasulu na maeneo mbalimbali kupata taarifa ili baadaye wajue wapi fursa zinapatikana.

Washiriki wakifuatilia kwa umakini maelezo kutoka kwa mkufunzi

Naye katibu mtendaji wa shirika la OHIDE Bi. Silesi Malli amesema kuwa mafunzo hayo yanayotolewa na kituo cha buha radio fm chini ya shirika la OHIDE ni sehemu ya mchakato wa ajira na kwamba watakaofanya vizuri baadaye wawe waandishi wa habari katika kituo hicho.

Kwa upande wao baadhi ya waandishi wa habari washiriki wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kukuza vipaji vyao ili baadaye kazi zao zisaidie jamii kujiunga na makundi mbalimbali ya kimaendeleo lakini pia jamii hiyo iwe inapata habari zenye ukweli na uhakika.

Shirika la ohide lilianza kufanya kazi zake mnamo mwaka 2015 na kusajiliwa rasmi julai 31, 2017 ambapo makao makuu yake yapo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma likiwa na dira ya kuhamasisha jamii katika masuala ya maendelo.

Shirika limefanikiwa kuanzisha kituo cha Buha radio  ikiwa ni mradi utakao saidia  jamii ya mkoa Kigoma  kuwa na chombo  rasimi cha mawasiliano ya umma ambacho  kitatumiwa na wananchi kujadili masuala ya maendeleo yao katika nyanja mbali mbali husasami elimu, uchumi, afya mazingira, utamaduni na sanaa na kukuza maendeleo kwa ujumla.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma