skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Giza totoro ni ishara ya mapambazuko .Aghalabu jogoo aliwika saa kumi  Alfajiri nilistuka kutoka usingizini na kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai huku nikisikia sauti za ndege angani

Niliamka na kujizoa kutoka pale kitandani nilipolala na kuelekea bafuni kuoga na kufanya maandalizi mengine  ya safari yangu ya kuelekea Kigoma ambapo nilitokea Natta mkoa wa Mwanza na kuelekea Kamanga kupanda Ferry na kuanza safari ya kuelekea Kasulu ambako nilikuwa naenda kwenye mafunzo ya uandishi wa Habari na Utangazaji katika lisilokuwa la kiserikali OHIDE linalomiliki kituo cha Buha Radio Fm sauti ya Kigoma.

Nikifurahi kuona Kibao kilichoniwezesha kufika kituo cha Buha FM na shirika la OHIDE mjini Kasulu

Natazama nikiwa safarini kuelekea Kigoma nimeona vitu mbalimbali ikiwemo mbuga ya Wanyama ya Muyowosi Kigosi,shughuli za kibiashara ambazo zinaongeza pato la taifa.

Safari yangu kuelekea BUHA ilikuwa na faida nyingi, kitambo nilisikia malumbano mitaan n ahata Bungeni viongoozi na wawakilishi wa wananchi wakiparuana kuhusu mitazamo ya Waha kuhusishwa na raia wa nchi Jirani hasa DRC na Burundi, malumbano hayo huacha maswali mengi lakini baada ya kufika katika eneo la Muyovozi mpakani mwa Kigoma na Kagera nimeshuhudia ukaguzi mkali wa vitambulisho vya Taifa hali iliyopelekea vijana wawili ambao sio raia wa Tanzania kuwekwa chini ya Ulinzi. Huenda hii ndiyo sababu mkoa wa Kigoma hutazamwa kwa jicho maalumu linapokuja suala la uhamiaji na wakimbizi. Ama kweli “Tembea uone” wanaosafiri kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam, au Dodoma hawakutani na Misako na ukaguzi mkali, wanaokabiliana na hili ni wanaopanda gari za abiria kutoka Kigoma, au kwenda Kigoma.

Muonekano wa Mji wa Kasulu kutokea mlima Sunzu ambako mitambo ya Buha FM itafungwa na kufikia mkoa mzima

Nikiwa nimewasili wilaya ya Kasulu kweli nimejionea uwekezaji mkubwa wa mashirika ya umma na yasiyo ya umma,biashara masaa ishirini nne ,maduka makubwa ya bidhaa za kilimo hakika Kasulu inavutia,ukarimu wa wenyeji wa mkoa wa Kigoma Pamoja na kufanya kazi kwa bidi ili kuongeza patao la taifa,

Safari yangu haikuishia hapo ambapo nimekutana na washiriki wenzangu kutoka mikoa mbalimbali Tanzania cha kwanza kabisa nilikuwa na hamu sana ya kujua nini cha kufanya na cha kujifunza juu ya tasnia nzima ya Habari, pili nimepata ushirikiano mkubwa sana kama kijana wa kike wa kipekee katika mafunzo hayo ambayo yamenipanua sana kifikra na kiutendaji katika kuaandaa vipindi vyenye weledi na kutangaza kwa umakini.

Kubwa zaidi nimekuwa wa kipekee na kimenipa thamani mimi kama mwanamke kuweza kucheza mchezo wa vishale [DARTS] japo haikuwa haba nilipambana katika mchezo huo na kufuzu kuingia nusu fainali ni jambo limenipa thamani sana na kujiona kumbe tukiamua tunaweza, hata mimi nazidi kushawishika moyoni kutoa hamasa kwa wanawake wenzangu na mabinti kwa ujumla kujituma na kujibiidisha kaika mambo mengine si michezo tu hata katika masuala mbalimbali ya kijamii.

Nikicheza mchezo wa Vishare kwa mara ya Kwanza tangu kuzaliwa, ama kweli Kasulu imenipa mambo

 Zaidi ya faida za mazoezi kwa mwanadamu ni nyingi zikiwemo kuimarisha afya ya akili dhidhi ya magonjwa nyemelezi, kuimarisha viungo na kuvifanya vyenye nguvu na kudhibiti matatizo  hasa uzeeni na kupunguza msongo wa mawazo.

Sitasahau suala la “fanya unachoona” huu ulikuwa ni mchezo wa sebene ulioletwa na mwezeshaji kwa ajili ya kutuondoa washiriki wote katika hofu, uchovu wa safari na mawazo ya namna ya kumudu mafunzo, yeye aliita kuwa ni mchezo wa kuvunja barafu, cha ajabu tulicheza sebene lililoongozwa na kibwezo (cartoon) lililoandaliwa maalumu kwa ajili ya kutuburudisha na kutuweka sawa. Kweli barafu iliyoganda katika hisia zangu za safari, ushuhuda wa wat una vitu uliyeyuka kama barafu na kujikuta nikisalia ukumbini na kuupa fursa ubongo wangu kuingiza mambo mapya.

Wahenga walisema hakuna marefu yasiyo na mwisho hata mbio za sakafuni huishia ukingoni tamati yangu nawasihi watanzania kuja kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Mkoa wa Kigoma.

Imeandaliwa na Matinde Nestory- Mwandishi kutoka Mwanza.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma