Na. Irene Bwire -PMO na Anita Balingilaki Buha - Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka…
Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar ndugu Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito kwa waislamu nchini kuutumia mfungo mtukufu wa Ramashani kupinga na kukemea vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi.
Rais hiyo ameitoa leo wakati akihutubia kongamano la kitaifa la kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani ambapo waislamu wanatarajia kuanza mfungo wa Ramadhani hivi karibuni baada ya mwezi kuandama
Ndugu Abdulla amebainisha kuwa vitendo vya rushwa vimekuwa na athari mbaya katika ustawi wa jamii na katika ukuaji wa uchumi, hivyo ni muhimu watu wote waungane kupinga vitendo hivyo
“Nawapongeza sana kamati ya kongamano la kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuandaa kongamano hili ambapo sote tumepata fursa ya kusikiliza mada mbalimbali kuhhusu athari za Rushwa na umhimu wa kuipiga vita” Amesisitiza Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar

mada mbalimbali zimetolewa na wanazuoni, viongozi wa taasisi za umma na viongozi wa dini kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa na uhujumu uchumi.
Mfungo mtukufu wa Ramadhani unatarajia kuanza hivi karibuni baada ya mwezi kuandama.
This Post Has 0 Comments