Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika inaadhimisha miaka 30 tangu kuasisiwa huku kukiwa…
Na. Mwandishi wetu,, Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya vituo kwa Mabalozi wawili (02) na uteuzi wa Balozi mmoja (01) kama ifuatavyo:
- Amempangia Balozi Humphrey Herson Polepole kuiwakilisha Tanzania nchini Cuba. Kabla ya uteuzi huu Balozi Polepole alikuwa Balozi wa Tanzania, nchini Malawi.

- Amemteua Balozi Lt. Jenerali (mstaafu) Yacoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE). Kabla ya uteuzi huu, Balozi Mohamed alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.
Uteuzi na kupangiwa Kituo
- Amemteua Bw. Iddi Seif Bakari kuwa Balozi na kumpangia Ubalozi nchini Uturuki. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Bakari alikuwa Konseli Mkuu, Dubai.