skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  
  • Azindua maduka ya uuzaji wa mbolea na kuhimiza vijana kujihusisha na kilimo
  • Aagiza wakuu wa wilaya, wakurugenzi na maafisa Ugani kuhamasisha wakulima kujiandikisha

Mbunge wa Kasulu mjini ambaye pia ni Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu kazi, ajira, vijana na wenye ukemavu Prof. Joyce Ndalichako leo amefungua na kushiriki mafunzo ya mawakala wa Pembejeo mkoa wa Kigoma.

Akihutubia wakati wa ufunguzi huo Profesa Ndalichako ametoa shukuranii za dhati kwa serikali na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapunguzia mzigo wa pembejeoo wakulima kufuatia kuweka ruzuku ya shilingi bilioni 150 kwenye mbolea.

Amebainisha kuwa wakulima katika jimbo lake la Kasulu Mjini kama ilivyo kwa wakulima wengine nchini walikuwa na ombwe kubwa la kupanda kwa bei za mbolea jambo ambalo lilikuwa linatishia ustawi wao pamoja na kuchangia kuporomoka kwa uchumi wa kaya, na kwamba kuwekwa kwa ruzuku kwenye mbolea ni fursa mhimu kwa wakulima kukuza kipato chao.

Mheshimiwa Ndalichako akihutubia umati wa mawakala wakati akizudua mafunzo akiwataka wawe waadilifu ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia

Mheshmiwa Rais ameupunguza mzigo mkubwa wa bei ya mbolea kwa wakulima, hii inatoa nafasi kwa kila mkulima kuongeza kasi ya uzalishaji, na ninaungana na wanahi wote nchini kutoa shukurani za dhati kwa mama yetu Samia Suluhu hassani kwa kuyaona mateso ya wakulima, Amlisisitiza profesa Ndalichako

Aidha Profesa Ndalichako ametoa wito kwa vijana kujitokeza katika shughuli za kilimo ili nao wanufaike na fursa zinazotolewa na serikali katika sekta ya kilimo ikiwemo ruzuku, huku akisisitiza kuwa wizara ya Kilimo pamoja na wizara anayoisimamia wameweka utaratibu mahususi wa kuwajengea uwezo vijana kiuchumi kupitia katika sekta ya Kilimo.

Wakati huo huo profesa Ndalichako amezindua maduka mawili makubwa ya uuzaji wa pembejeo yanayomilikiwa na makamapuni ya YALLA na ETG mjini Kasulu ambayo tayari yameanza kuuza mbolea kwa wakulima waliosajiliwa katika mfumo wa kidijitali.

Mh. Profesa Ndalichako akifurahia baada ya wakulima kujitokeza kununua mbolea ya ruzuku muda mfupi baada ya kuzindua uuzaji wake wilayani Kasulu.

Kwa mujibu wa kaimu meneja wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea kanda ya Kati Bw. Joshua Ng’ondya Mafunzo hayo yanalenga kuwapa elimu na uelewa wa taratibu mpya za mfumo wa ununuzi na usambazaji wa pembejeo hususani mbolea ya ruzuku iliyotolewa maelekezo na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupunguza gharama kwa wakulima nchini.

Bw. Ng’ondya ameweka bayana kuwa ili mkulima anufaike na mbolea ya ruzuku ni lazima awe amesajiliwa katika mfumo wa kidijitali ambao utamtambua kila mkulima aliyenunua mbolea pamoja na mashamba yao kutambulika na kusajiliwa.

Kuhusu mbolea ya ruzuku kutowanufaisha wakulima kutokana na mawakala na wakulima wenyewe kuuza nje ya nchi kama magendo Bw. Ngo’ndya amebainisha kuwa serikali imeweka utaratibu ambao utadhibiti utoroshaji kwa kushirikiana na vyombo vya dola pamoja na viongozi wa serikali za mitaa na kwamba mkulima, wakala au muuzaji atakayetorosha mbolea kwenda nchi za Jirani atashitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Kwa upande wao Issabella bakari na Justine kavuye ambao ni wakulima kutoka Kijiji cha Kanazi kata ya Ruhita ambao wamekuwa wa kwanza kununua mbolea ya ruzuku baada ya uzinduzi uliofanywa na Profesa Ndalichako, wamekili kuwa ruzuku iliyowekwa na serikali kwenye mbolea itawawezesha kuongeza mashamba na kulima kwa tija, kwakuwa kupanda kwa bei katika msimu uliopita ulisababisha kilimo kuwa cha wenye pesa huku maskini wakishindwa kununua mbolea ambayo awali iliuzwa kati ya shilingi laki moja na laki moja na therathini.

Kaimu Meneja wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea kanda ya Kati Bw. Joshua Ng’ondya akimuonesha mheshimiwa waziri Ndalichako namna mfumo wa uuzaji wa mbolea kidigitali unavyotumika.

Mafunzo hayo yamehusisha takribani mawakala 90 pamoja na Madiwani kutoka Halmashauri ya Mji wa Kasulu wameshiriki, hata hivyo mamlaka ya udhibiti imesajili mawakala wakubwa 40 katika mkoa wa Kigoma.

Asilimia takribani 90 ya wakazi wa mkoa wa Kigoma ni wakulima na mazao maarufu ya biashara na chakula ni mahindi, maharage, mhogo, alzeti, na michikichi.

This Post Has 0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma