skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Zainab Omary, Kigoma

Chama cha mapinduzi CCM kimefanya mabadiliko katika safu yake ya uongozi wa ngazi ya kamati kuu na Sekretarieti kwa kuwateua ziongozi kadhaa wapya huku wachache waliokuwemo wakiondolewa katika nafasi zao

Uteuzi huo umefanyika jana Januari 14 katika kikao maalumu cha halimashauri kuu kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam kikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Ndugu Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kikao hicho cha Kwanza cha Halmashauri kuu tangu kumalizika kwa uchaguzi wake mwezi Desemba mwaka 2022 kimemteua tena ndugu Daniel Chongolo kuendelea kuwa Katibu mkuu huku nafasi ya Naibu Katibu mkuu Bara iliyokuwa ikishikiliwa na Christina Mdeme akiteuliwa Anamringi Macha aliyewahi kushika nafasi mbalimbali za chama na serikali ikiwemo ukuu wa wilaya.

Ndugu Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi, na Rais wa Jamhurii ya Muungano wa Tanzania

Nafasi nyingine ni Katibu wa itikadi na uenezi taifa aliyokuwa nayo ndugu Shaka Hamudu Shaka sasa itaongozwa na Sophia Mjema ambaye kabla ya uteuzi wake alikuwa mkuu wa mkoawa Shinyanga.

Aidha Halmashauri kuu imemuondoa Kanali Lubinga katika nafasi yake ya Katibu wa NEC- Siasa na mahusiano ya kimataifa na nafasii yake imechukuliwa na Mbarouk Nassoroo Mbarouk.

Wakati huo huo Kikao hicho maalumu kimewateua wajumbe kadhaa wa kamatii kuu ambao watashirikiana na Ndugu Samia pamoja na Mwinyii kuongoza chama hichoo kikongwe katika kipindii cha miaka mitano (5) ijayo.

Waliochaguliwa ni Waziri mkuu msataafu Ndugu Peter Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Ndugu Nassoro Mwakasuvi, Halma Mamuya, Muhamed Mahamud, Nassri Ali, na Leila Ngozi.

Pamoja na uchaguzi huo ulioambatana na uteuzi, walioondolewa katika nafasi zao ambao ni SHaka Hamdu Shaka, kanali Lubinga na Christna Mdeme haijaelezwa sababu za kuondolewa kwaoo wala wapi watapelekwa. Hata hivyo watu wengi wamekuwa na mitazamo tofauti, wengi wakiamini kuwa huenda watapatiwa nafasi nyingine za uteuzi.

Makundi mbalimbali yanampongeza Mwenyekiti wa CCM Rais Samia kwa kuonesha ukomavu katika kupanga safu za chama wakidai kuwa nafasi za uongozi ndani ya CCM hazina hati miliki kwa makundi fulani ya viongozi, wakitaja kuwa mwenendo huo wa CCM ni ule aliouasisi Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Picha zote zimepatikana kwa hisani ya tovuti ya CCM

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma