Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Shirika la OHIDE Tanzania (Organization for Human Investment and Development) ambalo ndilo mwaasisi wa wazo la kuanzisha Radio ya BUHA FM, wamesajiri chama cha Ushirika kitakachotoa huduma za mawasiliano ya jamii (Community Internet Network)

Ushirika huo unatarajia kutoa huduma za internet kwa umma katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa lengoo la kurahisisha mawasiliano kwa umma.
Mwenyekiti wa ushirika huo uliopewa jina la Kasulu Community Network Cooperative Society LTD (KACONECOS) utasaidia jamii kupata huduma mbalimbali za kimtandaoo kwa njia rahisi na bei nafuu
KACONECOS inatarajia kushirikiana na Chuo kikuu cha Dodoma pamoja na Kondoa Community network kuomba leseni ya utoaji huduma za mawasiliano kutoka kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA.