Na. Mwandishi wetu, Kinshasa DRC Wakati Kanisa Katoliki nchini Tanzania likifanya ibada maalumu kumkumbuka Rais…
Nairobi, Kenya
Maafisa usalama kutoka Mataifa sita ya Afrika mashariki pamoja na nchi za ukanda wa pembe ya Afrika wamekutanishwa na Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na kudhibiti ugaidi (UNOCT) kwa kushirikiana na Jumuiya ya maendeleo ya ukanda wa kaskazini mwa afrika (IGAD) kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna sahihi ya kudhibiti misimamo mikali pamoja na ugaidi kwa njia ya mawasiliano chanya.

Katika warsha hiyo inayoendelea jijini Nairobi nchini Kenya mkakati mahususi unaozingatiwa ni utambuzi wa mbinu za mawasiliano zinazotumiwa na watu wenye misimamoo mikali wakiwemo magaidi pamoja na kubuni mfumo shirikishi wa namna ya kutoa simulizi zitakazosaidia jamii kutambua madhala ya ugadidi na kushiriki kudhibiti vitendo vya ugaidi
Miongoni mwa mambo yanayowekewa mikakati mahususii ya udhibiti ni mifumo ya mawasiliano na uwasilishaji wa ujumbe ambao utakuwa na tija kwa jamii ikiwemo kuyatambua makundii yaliyo katika hatari ya kushawishiwa kujiunga na makundi yenye misimamo mikali na makundi ya kigaidi
Aidha viongozi hao kutoka vyombo vya dola, asasi za kiraia na wanahabari wanajadili na kuweka mipango madhubuti ya namna vyombo vya habari vitavyoshirikiana na asasi za kiraia pamoja na serikali katika kutafiti, kuandika na kutangaza habari zinazohusu masuala ya usalama na kuelimisha umma kuhusu athari za uhalifu hususani ugaidi pamoja na majanga mengine kwa njia ya simulizi rafiki na zilizochambuliwa
Akizungumza katika warsha hiyo Bw. Craig Badings ambaye ni mtalaam wa mawasiliano ya migogoro na mshauri mwandamizi wa kituo cha udhibiti wa ugaidi Afrika, amesema ili kukomesha vitendo vya ugaidi suala la mawasiliano na namna ya kuwasilisha taarifa mbalimbali linapaswa kupewa kipaumbele zaidi kuliko mapambano.
“Kinachohitajika hapa ni uandaaji wa simulizi ambazo zitaleta mageuzi ya kifikira na mioyo miongoni mwa jamii na hasa vijana ambao ndio wanaoshawishiwa na magaidi ili washirikiane nao, magaidi wanatumia mbinu za mawasiliano, hivyo kubadili mitazamo hasi ni vema nasi tuwe na uelewa na ujuzi wa kuanzisha mawasiliano chanya na kutayarisha simulizi zitakazoleta mitazamo mipya ya kudhibiti jamii kuwa na misimamo mikali” amesisitiza Bw. Craig Badings
Moja ya changamoto zinazotajwa katika udhibiti wa vitendo vya ugaidi na kusabazwa kwa habari potofu zaidi kuliko zinazojenga jamii hasa katika mitandao ya kijamii ikiwepo Runinga za mitandaoni na Blog ambapo vijana wengi hata wasio na taaluma ya habari huanzisha chaneli zaoo nna kusambaza maudhui yenye upotoshaji na yasiyozingatia maadili na mawasiliano na habari.

Matukio ya ugaidi yanayoendelea katika nchi ya Msumbiji pamoja na Somalia pamoja na yale yaliyoripotiwa nchini Tanzania, Kenya na Uganda ni moja ya mifano inayotajwa kama kengele maalumu ya kuziamsha nchi za ukanda wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kaskazini mwa Afrika na Pembe Africa (IGAD) kuongeza juhudi za kukabiliana na makundi ya ugaidi kwa kuzingatia sababu na vyanzo vya matukio hayo
Rai hiyo imetolewa na Daktari Mustafa Ali ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya Arigatou International ambaye pia ni mwasisi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Pembe ya Afrika wakati akitoa mada kuhusu athari za mlipuko wa UVIKO 19 (COVID 19) na namna magaidi walivyoutumia ugonjwa huo kama fursa ya kushawishi jamii za kidini na kuchochea hisia kali na baadaye kutekeleza uhalifu

Daktari Mustafa amebainisha kuwa wakati jamii na mataifa ya Afrika wakihangaika kudhibiti ugonjwa wa Corona kwa upande wa magaidi waliitumia kama fursa ya kueneza ujumbe na simulizi za kupotosha zilizolenga kuwapa fursa ya kutekeleza uhalifu wao dhidi ya binadamu
“Wakati COVID 19 ilikuwa ni tishio duniani, magaidi walisambaza ujumbe wa kuzishambulia nchi mbalimbali ikiwemo Somalia, Msumbiji na Marekani wakidai kuwa ugonjwa huo ni Silaha kutoka kwa Mungu na Al Shaabab waliivamia Somalia na kambii ya Ulinzi wa amani ya umoja wa mataifa wakati ambapo kambi hiyo ilitumika kama kambi ya kusaidia waliobainika kuwa na maambukizi ya corona” Amesisitiza Daktari Mustafa


Washiriki wa warsha hiyo ya Umoja wa mataifa wamebaini kwa pamoja kuwa, ili kupambana na Ugaidi pamoja na kuwadhibiti watu wenye hisia na itikadi kali ni lazima kubuni mfumo imara wa upashanaji wa habari ambao utaamsha ari kwa jamii kushiriki kuzuia matukio hayo kwa kuwatambua wahusika pamoja na mikakati yao ambayo wakati mwingine hutumia majanga mengine kama fursa kwao
“Magaidi wana ujuzi wa hali ya juu unaotumika kuwashawishi vijana na watoto kujiunga nao na kisha kuwatumia kufanya vitendo vya kikatili, baadhi ya makundi ya Ugaidi yamefikia hatua ya kuwafundisha watoto wadogo kufanya mauaji na kishwa kuwanywesha damu ya binadamu iliyochanganywa na mitishamba huku wakiwalaghai kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa imara na hakuna kitakachowazuia kufanikisha azima yao, matendo kama haya ni ya kinyama na vijana walijiunga nao baada ya kupata taarifa zenye ushawishi kutoka kwa makundi ya ugaidi” Amesistiza Daktari Mustafa

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 120,000 wameripotiwa kuyakimbia makazi yao kwa sababu ya mashambulizi ya wapiganaji wanaojitaja kama kundi la jihadi kaskazini mwa Msumbiji huku wengi kati yao wakiishi na ulemavu, huki ikibainishwa kuwa asilimia zaidi ya 15 ya watu wameyahama makazi yao katika ghasia ambazo zimeharibu jimbo la Cabo Delgado tangu 2017.

Nchi zinazokutana kwa ajili ya kuweka mikakati ya kudhibiti ugaidi kwa njia ya mawasiliano na utoaji wa simulizi zenye tija kwa jamii ni pamoja na Djibouti, Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda na Somali ambazo kwa nyakati tofauti zimewahi kukumbwa na matukio ya uhalifu wa kigaidi.